Amina Omari, Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigela amerudisha kwa wananchi shamba lililokuwa linamilikiwa na mwekezaji ambaye ameshindwa kuliendeleza kwa muda wa miaka mitatu na kushindwa kulipa fidia kwa wananchi.
Shigela ametoa agizo la kurudishwa ka shamba hilo leo wakati akizungumzia na wananchi wa kata ya Kiomoni katika ziara yake ya kata kwa kata ya kusikiliza kero za wananchi wa Jiji la Tanga.
Amesema mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Hengya ilimilikishwa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 900 kwa ajili ya kujenga kiwanda.
“Hili eneo leo nalirudisha kwa wananchi haiwezekani kwa muda wa miaka mitatu wananchi zaidi ya 700 wanashindwa kulima na kufanya shughuli za maendeleo kwa ajili ya kusubiri fidia” amesema.
Awali wananchi wa eneo hilo walisema kuwa wamelazimika kuacha kulima baada ya kuelezwa kwamba eneo hilo limemilikishwa mwekezaji hivyo wasubiri fidia zao ili waweze kuhamishwa eneo jingine.