24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Pwani ahimiza watendaji kutumia takiwmu za Sensa kwa maendeleo

Na Gustafu Haule,Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amewaagiza watendaji waliopo katika Halmashauri pamoja na wataalamu mbalimbali kutumia takwimu za Sensa ya mwaka 2022 katika kuendeleza shughuli za kiuchumi na maendeleo zinazofanyika Mkoani humu.

Kunenge, ametoa kauli hiyo leo Mei 31, wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya kwa kamati za  sensa mkoa ,Sekretarieti ya mkoa na viongozi wengine yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa.

Mafunzo hayo yalikuwa chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)chini ya usimamizi wa kamishna wa Sensa Tanzania Bara Anna Makinda pamoja na Kamishna wa Sensa Zanzibar, Balozi Mohamed Hamza.

Kunenge,amesema kuwa takwimu za Sensa ni muhimu kwani zitasaidia kufanya maamuzi sahihi hasa katika kutoa na kuonyesha umuhimu wa fursa za kiuchumi pamoja na uwezo wake kiuzalishaji.

Amesema kutokana na umuhimu huo wa Sensa hapa nchini ni lazima watendaji watumie takwimu hizo katika kuwasaidia wananchi hasa katika kutatua changamoto zao.

“Nawapongeza Kamishna wote kwa kusimamia vizuri zoezi la Sensa na sisi Mkoa wa Pwani tunaahidi kuzitumia takwimu hizi kikamilifu katika kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema Kunenge.

Aidha, Kunenge ametumia nafasi hiyo kupongeza Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya na hasa katika kuhakikisha zoezi la Sensa linafanikiwa hapa nchini.

Kwa upande wake Kamishna wa Sensa Tanzania Bara, Anna Makinda amesema kuwa kufanikiwa kwa zoezi la Sensa hapa nchini kumechangiwa na wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya.

Makinda amesema kuwa baada ya zoezi hilo kumalizika sasa wanafanya mafunzo ya wataalamu na viongozi mbalimbali wa Mkoa ili kuleta umuhimu wa kutumia takwimu zilizopo.

Amesema, mafunzo hayo yameanza kutolewa katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dodoma, Morogoro, Lindi,Mtwara na Pwani lakini matarajio yake ni kuhakikisha mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 yanafika mikoa yote nchini.

Kwa upande wake ofisa wa Takwimu Taifa Omary Mwinyi,amesema Tanzania kuna watu milioni 61.7 huku MkoaPwani kukiwa na  jumla ya watu milioni 224,000 ikiwa ni ongezeko la watu 929,279 kutoka Sensa ya mwaka 2012.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles