23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Ndikilo jino kwa jino na mafataki

Na MWANDISHI WETU-PWANI

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanawapa msukosuko na kuwakamata waliohusika kuwapa mimba wanafunzi 16 na kusababisha kushindwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi .

Ameagiza baada ya kukamatwa kwa watu hao wasiachiwe na vyombo vya dola kama njia ya kuwakomesha kutotamba mitaani.

Pia amewataka wazazi na walezi kuacha kumaliza kesi za mimba za utotoni majumbani kwa kurubuniwa fedha ili kuwaachia huru wanaobainika kuwapa mimba watoto wao wa kike.

Hayo aliyasema juzi alipokuwa akizungumzia changamoto zinazosababisha kushuka kwa ufaulu.

Ndikilo alitoa maelekezo kutofanyika kwa masihara kwa wahusika watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Alisema wanafunzi 223 ambao ni sawa na asilimia 0.74 hawakufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba kutokana na utoro (149), mimba (16),ugonjwa (15), vifo (9) na sababu nyingine 34.

Alitaja tatizo jingine kuwa ni mdondoko suala ambalo linachangia kushusha taaluma.

“Tunakazi ya ziada kukabiliana na mdondoko mashuleni, tunalea watoto kuacha shule, wilayani Mkuranga mdondoko ulikuwa 67, Kibiti 36, Chalinze 36. Kisarawe wanne, Bagamoyo 12, Mafia wanne, Kibaha Mjini tisa na Kibaha Vijijini wanne,” alisema Ndikilo.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Theresia Mbando alisema idadi ya wahitimu waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 30,010 kati yao wavulana 14,304 na wasichana  15,706 lakini waliofanya mtihani huo ni watahiniwa 29,787 wakiwemo wavulana 14,182 na wasichana 15,605 sawa na asilimia 99.26.

Naye Ofisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Abdul Maulid alisema Halmashauri ya Chalinze waliopata mimba ni tisa, Mkuranga wanne, Bagamoyo mmoja, Kisarawe mmoja na Rufiji mmoja.

Hata hivyo alisema kuna kupanda kwa ufaulu kimkoa kutoka asilimia 66.9 mwaka jana hadi asilimia 77.79 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles