27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RC Mongella apokea miradi ya mil 114 ya mwekezaji

Na BENJAMIN MASESE-MAGU

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amekabidhiwa  miradi  nane iliyokamilika  yenye thamani Sh milioni 114.2 iliyotekelezwa naKampuni  ya Mbogo Mining & General Supply Ltd, huku akiwagiza wakuu wa wilaya kumlinda na kumpa msaada pale inapohitajika.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa  vyoo vya kisasa na vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Bukandwe wilayani Magu jana, ikiwa ni sehemu ya miradi yote, Mongela alisema  hajawahi kupokea fedha ama miradi ya wawekezaji  kama sehemu ya faida yake kwa wananchi inayofikia Sh milioni 100 ispokuwa  Mbogo Mining.

Alisema mara zote kiwango cha fedha zitokanazo  na faida ya  uwekezaji, huishia  Sh milioni 15  au zaidi kidogo, lakini kampuni hiyo meonyesha uzalendo na mfano kwa wengine.

Baadhi ya miradi iliyokabidhiwa, ni   vyumba  viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Ilendeja  na Bukandwe vilivyogharimu Sh milioni 90, matundu 12 ya  choo cha kisasa na mfano katika Mkoa wa Mwanza kilicho na kabati yenye vifaa vya taulo za kike kilichogharimu Sh milioni 10.7, ukarabati wa choo cha walimu Shule ya Ilendeja Sh milioni nne.

Mingine ni  ujenzi wa uzio na ununuzi wa samani katika kituo cha polisi Kisesa, ununuzi wa sare na vifaa vya michezo shule za msingi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Magu, ukarabati wa  madarasa shule Ilendeja na Bukandwe, madawati na misaada kwa wananchi pale inapotokea matatizo ya kijamii.

“Sote tumejionea vyoo vya kisasa vyenye makabati ya taulo za kike, hakuna shule ambayo ina vyoo na vifaa vile ispokuwai Bukandwe pekee hivyo naomba miundombinu hii itunzwe na wawekezaji wengine waige kilichofanywa na Mbogo Mining & General Supply Ltd,”alisema.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Mbogo Mining & General Supply Ltd, Barnabas Nibengo alisema aliamua kujenga maghala yake ya vilipuzi kwa sababu ya usalama na  jiografia ya mikoa anayosambaza  vifaa  vya shughuli hiyo.

Alisema licha ya shughuli zake kufanyika nje ya mkoa, anajitolea kuisaidia jamii kwa sababu ya ushirikiano mzuri  uliopo tangu ujenzi huo ulipofanyika mwaka 2014 ambapo wananchi walimpa ardhi bila masharti magumu na haijawahi kutokea mgogoro baina yake.

“Pamoja na ushirikiano uliopo ngazi ya kitongoji hadi taifa, tunaishauri Serikali kuwapa kipaumbele zaidi wawekezaji  katika kutoa kandarasi za miradi mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo kunaimarisha uzalendo na kutupatia nguvu na ari ya kufanya kazi,”alisema.

MWISHO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles