RC MGHWIRA AMKAANGA MBOWE

0
710

NA OMARY MLEKWA-HAI


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amezidi kumkaanga Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kusema kuwa hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa kuondoa miundombinu ya umwagiliaji  katika shamba la Kilimanjaro Veggie si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji

Kauli hiyo aliitoa jana wilayani hapa baada ya kutembelea shamba hilo lililopo katika Kijiji cha Nshara ambapo aliojionea uharibifu wa mazingira   uliofanywa katika eneo hilo linalomilikiwa na Mbowe.

Alisema hatua zilizochukuliwa na DC huyo pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni sahihi kwani imelenga kulinda vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili kwa mujibu wa Sheria ya Mzingira ya mwaka 2004.

“Sheria iko wazi inasema kuwa tusifanye shughuli zozote za kibinadamu zenye madhara kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kwa mujibu wa sheria na shughuli hii ina madhara makubwa kwa mazingira na hata kwa binadamu,

“Shughuli hii nzuri  na ni uwekezaji mkubwa ninavyofahamu kilimo cha stobeli kikishatema maji lazima yaende mahali hata kama unatumia umwagiliaji wa kisasa wa matone ya maji na yanakuwa na madhara kwa binadamu wanaotumia maji hayo.

“…jambo hili mmiliki wa shamba alikubali na kukiri kuwa ni kosa kisheria  na kukubali kuondoa mazao yake mpaka Mei 23, mwaka huu baada ya kukubaliana na Mkuu wa Wilaya ya Hai atatumia miezi minne kuondoa mazao yake lakini hakufanya hivyo na badala yake ameanzisha kulima mazao mapya,” alisema RC Mghwira.

Alisema Mbowe aliwahi kuomba viongozi wa mkoa katika kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kiitishwe ili kuweza kujadili suala la mazingira na umuhimu wa kuheshimu sheria za mazingira ambapo kikao hicho kiliketi na kubaini ni kwa nini kiongozi huyo alishindwa kuheshimu.

“Yeye ni kiongozi angetusadia kuelimisha wananchi kuhusu kuheshimi sheria  lakini amekuwa wa kwanza kuzivunja  na serikali imeweka sharia ya mita 60 kusifanyike shughuli za kibiadamu ,”alisistiza

Alifafanua kuwa endapo mazingira yatatunzwa vizuri kila kitu kitafanyika kwa ufasaha na kutokutunza mazingira kumechangia kupelekea kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kutokana na kutegemea sana utunzaji vyanzo vya maji katika kutunza mazingira .

Kutokana na hali hiyo RC Mghwira alisisitiza kutokuendelea kwa shughuli zozote za kibinadamu katika shamba hilo kwani mmiliki alikwishakiri kufanya kosa na kupewa adhabu ya kulipa kiashi cha Sh milioni 18.

“Tunapenda uwekezaji katika maeneo yetu kwani zimechangia sana ajira  lakini zifanyike kwa kufuata taratibu  na sharia za nchi ili kuondokana na migongano  na wawekezaji,”.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nshara, Clement Kwayu (Chadema), alimwomba RC Mghwira, kuruhusu kuendelea kwa kilimo hicho katika eneo hilo kwani kimesaidia kutoa ajira kwa vijana  zaidi ya 50 na pia eneo hilo ni la asili na wameweza kulima kwa zaidi ya miaka 40.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here