29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

RC Mbeya: Watu wasiojulikana wanatafuta uhai wangu

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema watuwasiojulikana wanatafuta uhai wake.

Chalamila alisema kutokana na kuwapo mazingira hayo, ametangaza vita dhidi ya watu hao, huku akiwataka wajisalimishe haraka polisi.

Alisema watu hao walifika na gari nyumbani kwake eneo la Uzunguni jijini hapa na kuwakabidhi walinzi vifurushi vya mchele  ambao ulibainika kuwekwa sumu iliyokusudiwa kumuangamiza yeye na familia yake.

Chalamila aliyasema hayo jana wakati akizungumza na maelfu ya wanachama wa Chama cha Mapiduzi (CCM) pamoja na wakazi wa Jiji la Mbeya waliojitokeza kwenye maandamano ya amani ya  kumpongeza Rais Dk. John Magufuri kwa kazi nzuri ya maendeleo anayoifanya nchini .

Maandamano hayo ambayo yalianzia kwenye viwanja vya Rwanda Nzovwe na kuishia Ofisi ya  CCM Wilaya ya Mbeya iliyopo eneo la Sabasaba yaliungwa mkono na wananchi, viongozi na watumishi wa umma.

Alisema anashangazwa kuona watu wakifuatilia maisha yake kwani binafsi hataweza kubadili mfumo wa utendaji kazi wake wa kutetea na kupigania haki za wananchi ikiwapo kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kama Rais anavyotaka.

“Wiki hii kuna gari lilifika nyumbani likiwa na rangi nyekundu, lilikabidhi vifurushi vya mchele kwa walinzi lakini ulipochunguzwa ulibainika kuwa umewekwa sumu yenye madhara kwa afya yake na familia na kusudi kubwa ni kutaka kumuua jambo ambalo halitawezekana,”alisema.

Aliwataka watu hao kutambua kwamba yeye amechaguliwa na kuteuliwa na Rais kuongoza mkoa  huo kwa maana kubwa sana hivyo njama za kuondoa uhai wake hazitafanikiwa na kwamba jaribio hilo ndio limemfanya kutangaza vita hadharani na wauaji hao.

“Kila kitu kinasababu yake, mimi kupewa uongozi nikiwa na miaka michache kuna maana yake nilikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Rais ameniona na kunipa Mkoa, hivyo sitakubali kamwe uhai wangu uondolewe na watu wenye nia mbaya na maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles