22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

RC Makalla: Rais Samia ni kielelezo sahihi cha Muungano

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Muungano wa Tanzania ni wa mfano duniani, haujawahi kuterereka Na chini ya Rais Dk. Samia utaendelea kuimarika na mafanikio lukuki ikiwemo miradi mikibwa ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano yaliyofanyika viwanja vya Zakheem Mbagala Aprili 26, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuna maendeleo na mafanikio makubwa yaliyofanyika.

“Rais Dk. Samia amesaidia mwendokasi ifike mpaka Vikindu, fedha Sh bilioni 9 kujenga Hospitali Mbagala Kuu na A, hivyo anawataka wananchi kuenzi na kulinda muungano huu,”amesema Makalla.

Amesema kuhusu suala la kero za Muungano Rais Dk. Samia anaendelea kuzishughulikia hadi sasa.

“Katika maadhimisho haya nawaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Meya wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya Kusini unafanyika. Pia ametoa kiasi cha Sh bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mbagala Kuu,” amesema Makalla.

Makalla amesema maadhimisho hayo Kimkoa yameenda sambamba na uzinduzi na uwekezaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 23.

Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles