RC KUPAMBANA NA WALIMU MAFATAKI Z’BAR

0
2230

Na KHAMIS SHARIF,ZANZIBAR   Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema walimu wakware kwa watoto wa kike watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema tangazo lake hilo linalenga kuwafahamisha walimu kuwa sasa umefika mwisho wa kuvumilia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi hasa wanapokuwa nje ya shule.

Akizungumzia jana wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa kikapu, Ayoub alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imejipanga kukomesha vitendo vya udhalilishaji.

Alisema inasikitisha taifa kushindwa kupiga hatua ya maendeleo kutoka na wananchi wake kuathiriwa na mambo mbalimbali ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, ndoa za utotoni na udhalikishaji wa kijinsia.

“Mwanafunzi ni sawa na mtoto wako nyumbani hivyo hakuna sababu ya kumshawishi kwa namna yoyote na mkifanya hivyo nitakula nanyi sahani moja hadi kieleweke,” alisema Ayoub.

Aliwataka wazazi kusimamia vyema mienendo ya watoto wao wanapokuwa shuleni na nyumbani ili waepuke athari za vishawishi hatarishi ambavyo ni tishio kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here