25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kilimanjaro aitaka Kenya kuwaachia Watanzania

Safina Sarwatt, Rombo

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira amemwagiza Mkuu wilaya ya Taita Taveta nchini Kenya kuwaachia huru Watanzania saba wanaoshikiliwa nchini humo kwa zaidi siku 14 kwa makosa mawili ya kutovaa barakoa na kuingia bila kibali.

Akuzungumza leo Januari 18, mara baada kikao cha kutafuta suluhu iliyoshirikisha pande zote mbili ya Tanzania na Kenya kilichofanyika katika mpaka Holili wilayani Rombo na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya za Taita Taveta, Rombo, Mwanga na Moshi.

Dk. Mghwira amesema kuwa kikao hicho ni kuhusiana na kushikiliwa waendesha boda boda raia wa Tanzania 15 walioshikiliwa Taveta kwa makosa mawili ambapo nane walifanikiwa kutoka baada kutimiza masharti huku wengine saba walishindwa kutimiza masharti hayo.

Amesema kuwa baada kukamatwa walipigwa faini kwa kila kosa ambapo kosa la kwanza ni yakuingia bila kibali ambayo faini yake ni Sh za Kenya 20,000 kosa la pili kutovaa barakoa Sh za Kenya 30,000 sawa Sh million moja ya Tanzania.

“Tumekaa tukajadili lakini tumeona ni makosa tu yakawaida ya kimazoea ya kibiashara kwasababu Wakenya wanaingia bila kufuata taratibu tena bila masharti wanachukua bidhaa lakini Watanzania wakiingia tu upande wa Kenya ni kosa, “amesema Dk. Mghwira.

Dk. Mghwira amemtaka Mkuu huyo wilaya Taita Taveta, Joseph Maina, kuwasiliana na waendesha mashtaka ili kuona namna yakuwaachia huru Watanzania hao bila masharti yoyote na endapo ilishindikana hatua nyingine ifuatwe na hata kama ikiwezekana iendeshwe mahakama ya wazi.

“Makosa hayo ni makosa tu ya kibishara kama ambavyo boda boda za Taveta wanaingia upande kwa kwetu na abiria bila masharti kuvaa barakoa wala kibali hilo halikubaliki kuwepo kwa usawa pande zote mbili,” amesema.

Amesema biashara ya mipakani ni nyingi hivyo waweke utaratibu wa kufanya biashara kama kuna sheria zifuatwe na pande zote mbili, kwani serikali halitaweza kulifumbia macho suala hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Taita Taveta, Maina amesema kuwa wiki mbili zilizopita kulitokea kutofautia kidogo sisi na majira zetu na leo tukaa tafuta suluhu lakini haikupatikana na kikao hicho kimeahirishwa.

Naye Mkuu wa wilaya Rombo, Dk. Athuman Kihamia amesema wamepokea maelekezo ya mkuu yeye pamoja na wakuu wa wilaya wenzake na kwenda kulifanyia kazi ili kupata suluhu ya pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles