30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kagera azitaka Halmashauri kutenga asilimia ya pato la kahawa kuzalisha miche

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Alberth Chalamila ametoa wito kwa Halmashauri zote mkoani Kagera kuhakikisha zinatenga asilimia 20 itokanayo na kodi ya Kahawa (Sesi) inarudi kuzalisha miche bora ya kahawa ili kujiepesha na miche ambayo siyo bora inayoweza kuzalishwa kutoka nje ya nchi.

Chalamila ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua semina ya mafunzo kwa viongozi vya vyama vya msingi (AMCOS) yaliyoandaliwa na Tume ya Ushindani Tanzania(FCC) ambayo yalilenga kujenga uelewa kwa viongozi wa vyama vya msingi na wale wa ushiriki juu ya majukumu ya tume.

Amesema katika msimu huu wa kahawa 2021/2022 tayari Halmashauri za mkoa wa Kagera zimepokea mapato yatokanayo na zao hilo lakini atashangazwa kuona hakuna shukurani inayorudi kwa wakulima.

Ameongeza kuwa kunautamaduni ambao umejengeka kuwa mbegu kutoka nje ya nchi ndizo bora wakati ndani ya halmashauri na tasisi kuna wataalamu ambao wanaweza kuzalisha mbegu bora zinazoweza kumsaidia mkulima kupata mavuno.

“Nitumie nafasi hii kwataka Wakurugenzi mhakikishe asilimia 20 ya mapato ya kahawa inarudi kwa wakulima wenu kwa sababu wao ni sehemu ya kipato hicho, nisingependa kuona halmashauri haina vitaru vya miche ya kahawa na miche hiyo wakulima waipate bure ili wavune zaidi, mfano nimeona Kyerwa mpaka sasa mmepata Sh milioni 900 ya kahawa Karagwe zaidi ya Sh millioni 500,” amesema Chalamila.

Amevitaka viwanda vinavyokoboa na kusaga kahawa ya unga kuongeza ubunifu katika bidhaa ya zao hilo iliyokobolewa ili kupata masoko zaidi kwani amegundua kuwa viwanda vingi vinavyouza Kahawa iliyoongezewa thamani vinaendana na mtindo wa zamani na hakuna ubunifu wowote katika bidhaa hiyo ya unga.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa FCC, Magdarena Utto amesema kuwa majukumu makubwa ya tume hiyo ni kulinda biashara, kumlinda mraji na kukuza uchumi.

Pia Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushilika Mkoani Kagera (KCU)1990 Ltd, Respicius John amesema hivi sasa tatizo la bei limetatuliwa kutoka Sh 1,400 hadi Sh 2,215 kwa kilo moja kahawa ya maganda aina ya Robusta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles