25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

RC: DC wachukulie hatua viongozi wa vijiji

AMON MTEGA-SONGEA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet  Mgema kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi wa vijiji na kata ambao maeneo yao yatakumbwa na  uchomaji moto na uvamizi wa  kwenye vyanzo vya maji kwa ajiri ya shughuli za kibinadamu kinyume na taratibu.

 Agizo hilo, alilitoa hivi karibuni baada ya kusomewa taarifa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), alipotembelea shamba la kahawa lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 3,000 ambalo linamilikiwa na mwekezaji wa Kampuni ya AVIV lililopo Kijiji cha Matomondo Songea Vijijini.

Mndeme. akipokea taarifa hiyo iliyohusu malalamiko kutoka kwa mwekezaji  kuwa wananchi wamekuwa wakivamia vyanzo vya maji vilivyopo kwenye milima ya Litenga ,jambo ambalo limekuwa linasababisha kupungua kwa maji ya Mto Ruvuma.

Alisema kumekuwapo na tabia ya uharibifu mkubwa wa mazingira, ikiwamo ukataji wa miti na uchomaji moto ovyo wa misitu, huku viongozi wa vijiji na kata, wakiangalia bila kuwachukulia hatua wahusika.

Alisema ipo tabia ya viongozi kama watendaji wa vijiji,kata na madiwani ambao wamekuwa wakiona matukio ya uchomaji moto kwenye maeneo yao, lakini hakuna hatua wanazochukuwa.

“Nakuagiza mkuu wa wilaya  kuanzia sasa, tukio la moto ukitokea kijijini,viongozi wachukuliwe hatua za kisheria,wao wanawajua wahusika wa vitendo hivi,” “alisema.

Aliagiza TFS kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira, kwani inaonekana wengi hawajui umuhimu wake.

Wakati huo huo, aliwaagiza makatibu tarafa wote wa wilaya hiyo kuwachukulia hatua watu wote ambao wamejenga kwenye vyanzo vya maji ili kuvinusuru kukauka na kusababisha wananchi waingie kwenye janga la ukosefu wa maji.

 Alisema kiutaalamu maeneo ya vyanzo vya maji hayapaswi kuwekwa makazi ya watu,yanaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwamo magonjwa ya mlipuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles