23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RC Chalamila ahimiza ushirikiano Kagera

Na Renatha Kipaka, Bukoba

MKUU wa Mkoa Kagera, Albert Chalamila amewataka watumishi mkoani humo kumpa ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa watu wote.

Chalamila ameyasema hayo Agosti 5, 2022 mjini Bukoba wakati akizungumza na watumishi mkoani humo baada ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Charles Mbuge.

Amesema wapo wafanyafanyakazi wanaofanya vizuri na wengine wanafanya mzaha.
“Wengine wapo kwa ajili ya utani wanaona kama haujafanya kazi, mtu akijitoa akafanya kwa maendeleo ya wananchi wengine atasema hajafanya chochote,”amesema Chalamila.

Chalamila amesema hakuna sababu ya kuanza kutotekeleza majukumu nakwamba jambo la msingi ni kufanyakazi kwa juhudi na ushirikiano.

Awali, Meja Jen. Mbuge alisema kuwa katika utumishi wake kwa nafasi hiyo alisimamia miradi ya maendeleo kwenye mkoa huo.

Mbuge aliongeza kuwa, imani kubwa miradi hiyo itaendelea ikiwa ni pamoja na kuimarisha zao la kahawa, mradi wa bomba la mafuta na shughuli ya sensa itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu.

Ameongeza kuwa, katika Halmsahauri kuna ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na kulipatia taifa uchumi.

Akitoa neno kwa watumishi Katibu Tawala wa Mkoa huo, Toba Nguvila amesema amepata nafasi ya kutumika nakwamba ataitumia vizuri na kuwa tayari kupokea ushauri kwa mtu yeyote.

“Nipo tayari kutumikia watumishi na wananchi wa mkoa huu, na kuendelea kushirikiana na wakuu wa wilaya katika nyanja mbalimbali ili kuimalisha uchumi wa mkoa wetu wa Kagera,” amesema Nguvila na kuongeza kuwa:

“Nilipokuwa mkuu wa wilaya ya Muleba, tulikuwa tunaleta matatizo yetu hapa mkoani yatatuliwe sasa ndugu zangu Ma-DC(Wakuu wa Wilaya) mimi nipo hapa tutashirikiana,” amesema Nguvila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles