24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC AZUIA USAFIRISHAJI CHAKULA USIKU

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Kilimanjaro, Anna Mghwira

Na UPENDO MOSHA – MOSHI

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imepiga marufuku usafirishaji wa mazao ya nafaka na sukari wakati wa usiku.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa (RC) wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, alisema ofisi yake imejiridhisha kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha mazao ya nafaka na sukari nyakati za usiku kupitia njia zisizo rasmi, huku wakishirikiana na baadhi ya askari polisi wasiokuwa waaminifu.

“Ni marufuku kusafirisha sukari, mchele, mahindi, mpunga na unga wa mahindi kutoka mkoani Kilimanjaro nyakati za usiku kwani wengi wamekuwa wakitumia mwanya huo kusafirisha mazao hayo kwenda nje ya nchi.

“Mfanyabiashara yeyote atakayekamatwa akisafirisha mazao hayo wakati wa usiku, atachukuliwa hatua kupitia sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200.

“Pia, mali ya mtuhumiwa itataifishwa na kupelekwa kwenye ghala la chakula la taifa kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alilolitoa Juni 26, mwaka huu, wakati wa Baraza la Idd lililofanyika mjini Moshi, mkoani hapa,” alisema Mghwira.

Wakati huo huo, mkuu huyo wa mkoa, aliwataka askari polisi wanaojihusisha na shughuli za usindikizaji na kupanga njia za kusafirisha mazao hayo, waache tabia hiyo kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Pia, aliitaka Idara ya Uhamiaji mkoani hapa, kufanya uchunguzi wa kuwabaini wafanyabiashara kutoka nje ya nchi, ambao wamekuwa wakiingia nchini na kujihusisha na ununuzi wa mazao yakiwa mashambani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles