23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC AWATAKA WALIOSAHAULIKA KWENYE FIDIA KUTOA TAARIFA SAHIHI


Na AMON MTEGA
-SONGEA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, amewataka wakazi
waliosahaulika kwenye malipo ya fidia ya kupisha mradi wa maji katika Bonde la Mto Luhila mkoani humo,
kutoa taarifa sahihi ili zoezi la uhakiki lifanyike kwa wakati.

Akizungumza juzi na wadai hao kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika
katika viwanja vya Shule ya Msingi Luhilaseko, alisema wakazi waliothaminiwa ni 803 na kwamba wadai waliosahaulika ni 194 na mirathi
kwa ndugu waliofariki ni 121.

 

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha
kila ambaye anastahili kupewa haki yake anapewa bila upendeleo, hivyo
pasitokee wa kufanya udanganyifu wakati wa uhakiki wa
taarifa,” alisema Mndeme.

Alisema watu ambao tayari taarifa zao zimekamilika, wataanza
kulipwa hivi karibuni huku
akiwaagiza wataalamu kuhakikisha zoezi la malipo linafanywa kwa uangalifu
mkubwa ili kuepusha malalamiko.

 

Naye Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dk. Damas Ndumbaro (CCM), alisema fedha zinazotakiwa kulipwa ni zaidi ya Sh bilioni moja na kwamba fedha za awali zilizopatikana ni Sh milioni 500 ambazo zitaanza kulipwa wakati mchakato wa kuingiza fedha nyingine ukiendelea.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Songea (SOUWASA), Patrick Kibasa, alisema watajitahidi ili kuhakikisha mwishoni mwa mwezi huu wadai wa awali wawe wamelipwa.

Mmoja wa wadai hao, Amidu Maniamba, alisema walipisha mradi huo zaidi ya miaka mitano, hivyo aliiomba Serikali pamoja na kuwalipa fidia wawatatulie kero ya maji ambayo inawafanya
wafuate maji umbali mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles