27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

RC ATOA WIKI MBILI KWA WALIOTAFUNA FEDHA ZA USHIRIKA

Na Mwandishi Wetu-Kibaha


MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, ametoa wiki mbili kwa vyama vya ushirika vya msingi vya korosho vya Rufiji, Kibiti na Mkuranga kufika ofisini kwake na kujieleza kwa nini visichukuliwe hatua kutokana na upotevu wa mamilioni ya fedha za wakulima.

Kauli hiyo aliitoa juzi alipozungumza na viongozi wa vyama vya Ushirika Msingi wa Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga.

Alisema ni lazima sheria ifuatwe katika kulinda fedha za mkulima mdogo wa kawaida.

  Mkuu huyo wa mkoa alieleza jinsi  Bungu B Amcos  ambao walimuuzia mnunuzi tani 320 ambako alikuta 298 huku  tani 22 zikiwa hazipo zenye gharama ya Sh milioni 72.9.

“Bungu Amcos mnunuzi alikuta tani 11 hazipo zenye thamani ya Sh milioni 33. Bungu Mahege Sh milioni 12 zimetiwa mfukoni, Mjawa Amcos tani 4 zimepigwa zilizogharimu Sh milioni 11,” alisema Ndikilo.

Alisema hawezi kukubali kuona vyama vya ushirika vinashiriki kuupa Mkoa wa Pwani  fedheha na sifa mbaya kwa taifa.

Alisema vyama vilivyojihusisha utapeli dhidi ya wanunuzi vitoe sababu za msingi kwa wakuu wa wilaya kueleza ubadhirifu huo na wakibainika kufanya wizi vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani, aliomba utumike vizuri kwa sababu  bila kufanya hivyo utateteleka.

Ndikilo alisema ni lazima haki itendeke wakulima wanufaike badala ya kuwabana kwa kuwapa masharti magumu hali itakayosababisha kuondoa imani na mfumo huo ambao ndiyo unawanufaisha kwa sasa.

 “Safari hiii atakaebainika kufanya ujanja ujanja tutamfunga, na hapo ndipo mtajua kama mna RC (Mkuu wa Mkoa),  mkali, msile jasho la wanyonge ,”alisema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles