RC ATAKA VIONGOZI WAZIDI KULIOMBEA TAIFA

0
481

Na PETER FABIAN

MKUU wa Mkoa wa Mwanza (RC), John Mongella amewataka viongozi wa dini zote wasichoke kuliombea taifa liendelee kuwa na amani.

Vilevile aliwataka wamombee Rais Dk John Magufuli ambaye ameamua kuwa mzalendo wa kuhakikisha anapambana na wezi wa rasilimali zote  ziweze kuwanufaisha watanzania bila kwabagua  ili kuwaletea maendeleo ya kweli katika uchumi.

Mongella alikuwa mgeni rasmi kwenye futari iliyoandaliwa juzi na mfanyabiashara maarufu wa Mwanza, Christopher Gachuma ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM   kutoka Wilaya ya Tarime.

Alimshukuru Gachuma kwa kuwa na utaratibu wa kufuturisha kila mwaka kwa lengo la kuwakumbusha viongozi mbalimbali wa dini, serikali na wanasiasa kuwa umoja na ushirikiano ndiyo nguzo ya misingi ya amani kwa mkoa wa Mwanza na nchini kwa ujumla.

“Tufanye kazi hii kila wakati na kuhakikisha watanzania kwa pamoja wanaendelea kuliombea taifa na Rais Dk. Magufuli ambaye ameonyesha uzalendo wa kupigania haki ya rasilimali za taifa  zitumike katika kukuza uchumi na kureta maendeleo kwa watanzania bila kuwabagua.

“Hiyo ni kwa kuzingatia vita ya uchumi duniani kote hupingwa kwa nguvu na mabepari,”alisema.

Mongella alisema  ni vema viongozi wa serikali waliopewa dhamana ya kuwasimamia wananchi wakawa  wenye maono ya kushirikiana na viongozi wa dini zote I kusaidia wananchi kutokubali kudanganywa na wachache kwa masilahi yao.

Naye  Gachuma alisema utaratibu  huo unalenga kuwakumbusha ushirikiano bila kujali dini, kabila na itkadi za  siasa bali kuwa wamoja na kuendelea kutenda mema yanayotokana na dini zote ili kudumisha amani na umoja wa Mkoa na taifa kwa ujumla.

Shekh Hassan Kabeke aliwaasa   viongozi wa dini zote kuwa mstari wa mbele kuwaongoza wananchi kumwombea Rais D.k Magufuli na taifa kwa ujumla  kushinda vita kubwa ya kupigania uchumi na maendeleo ya taifa.

Askofu Zenobius Isaya wa Makanisa ya Pentekoste ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza alimpongeza Rais Dk Magufuli kwa kuwa mzalendo aliyethubutu kulinda rasilimali za taifa.

Vilevile alimpongeza Gachuma kwa kutimiza jukumu la kuwakutanisha viongozi na waumini wa dini zote  na viongozi wa serikali na vyama vya siasa katika futari ikiwa ni kudumisha umoja na mshikamano ndani ya mkoa na wilaya zake kwa misingi ya amani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here