31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RC asikitishwa ongezeko vitendo vya ubakaji

TIMOTHY ITEMBE

MKUU wa Mkoa Mara, Adam  Malima ametaja sababu za kuongezeka matukio ya ubakaji kwa  kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu.

Amesema hiyo inatokana na baadhi ya walimu wasiokuwa na maadili kuwafanyia wanafunzi wao vitendo hivyo pamoja na waendesha pikipiki maarufu (bodaboda).

Malima alisema  kipindi cha Januari hadio Mei mwaka huu kuna matukio ya vitendo vya ubakaji zaidi ya 12 vimeripotiwa ofisini kwake ili kuvishugulikia na kupatiwa ufumbuzi.

Alisema waathirika katika vitendo hivyo ni wanafunzi wa shule za misngi na sekondari.

RC alitaja ongezeko la vitendo hivyo kuwa vinachangiwa na baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari  na waendesha pikipiki.

Matukio ya ukatili na ubakaji yakiwamo ya ulawiti ni miongoni mwa ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu   na utawala bora nchini.

Alisema  kuenea kwa vitendo hivyo kunasababisha uzorotaji maendeleo kwa taifa.

 “Ofisini kwangu kumeripotiwa kesi za ubakaji zaidi ya 12 baadhi zikiwa zinahusisha walimu wa shule za misngi na sekondari.

“Niwaombe ndugu zangu haki ya kufanya kazi  bila kubugudhiwa ni ya msingi lakini niwatake kuacha vitendo vya rushwa ya ngono kazini pamoja na vitendo vya ubakaji watoto wa shule,” alisema Malima.

RC alitaja vipaumbele katika mkoa   kuwa ni elimu, afya, miundombinu ya barabara   na maji.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania Mkoa Mara,   Livingstone Gamba aliwataka walimu   na wafanyakazi kwa ujumla kuchukua wajibu wa kufanyakazi kama sheria inavyowataka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles