23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

RC ARUSHA AWATEGA MA-DC

 MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema hatomwelewa wala kumwonea haya mkuu wa wilaya ambaye halmashauri yake itapata hati chafu au ya shaka kwa hesabu za mwaka jana.

Kutokana na agizo hilo, aliwataka kwenda kusimamia hoja zote zilizowasilishwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 kabla ya mwisho wa wiki hii.

Agizo hilo alilitoa mjini hapa juzi wakati wa kikao cha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2017/2018 na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Akizungumza katika kikao hicho kilichohusisha halmashauri zote saba za Arusha na wataalamu kutoka ofisi ya CAG, Gambo aliitaka kila halmashauri kujibu hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi.

“Naagiza kila halmashauri ikamilishe ujibuji hoja kwa wakati na majibu sahihi si majibu yatakayoibua hoja au kutojitosheleza.

“Kwa halmashauri iliyopata hati chafu au ya shaka kwa mwaka wa fedha uliopita, iainishe wataalamu waliosababisha kupata hati hizo ili wachukuliwe hatua stahiki,” alisema Gambo.

Pia aliwakumbusha wajibu wao na kuwataka washiriki kikamilifu kuhakikisha hoja zinajibiwa ipasavyo, na kwa waliosababisha hoja hizo kwa kipindi cha nyuma wachukuliwe hatua ili kuleta nidhamu na kuongeza umakini.

Kuhusu asilimia 10 ya mapato ya halmashauri yanayotakiwa kutolewa kama mkopo kwa vikundi vya wanawake na vijana, alizitaka halmashauri ambazo hazijatoa asilimia hiyo zitekeleze agizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles