28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

RC AKASIRISHWA KUFUNGWA SHULE 11 KWA KUKOSA VYOO

Na JUDITH NYANGE – MWANZA


MKUU  wa  Mkoa wa Mwanza,  John Mongella,  amekasirishwa na kitendo cha Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya  ya Ukerewe  kufunga shule za msingi 11 kwa kukosa vyoo.

Pia ametaka kukutana na viongozi wote wa Ukerewe   na kamati inayowahusisha wakuu wa idara wa wilaya hiyo    waweze kumweleza ni sababu  zipi zilizowafanya kufunga shule zote  hizo.

Hayo yalibainika jana kwenye  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC) wakati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati,  alipowasilisha hoja ya maombi ya bajeti maalumu.

Akiwasilisha hoja ya maombi maalumu ya wilaya hiyo, Bahati  alisema uongozi ulilazimika kuzifunga shule hizo kutokana na ukosefu wa vyoo.

Alisema katika bajeti hiyo ya maombi maalumu  wilaya inaomba  Sh bilioni 8.1  kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule hizo zilizofungwa ziweze kujengewa vyoo kabla ya kufunguliwa.

 RC Mongella alishangazwa na kauli hiyo kwa kumkatisha   Bahati  na kumhoji ni wapi walipowahamishia wanafunzi waliokuwa wakisoma katika shule hizo 11 za msingi na nani aliyempa kibali  cha kufunga  shule hizo.

Alijibu swali hilo,  Bahati alisema wanafunzi hao kwa  wapo nyumbani tangu   shule hizo zifungwe. 

"Sheria ya elimu inasema hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kufunga shule  isipokuwa Kamishna wa Elimu pekee.

“Hata Rais au waziri  wa elimu hawezi kufanya hivyo lazima ashauriane na kamishna  kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

"Nyie mmefunga hizo shule kwa kibali au ruhusa ya nani  DC Ukerewe una hizi  taarifa?  Maana mimi mwenyewe ninayetakiwa kumshauri kamishna kufanya hivyo ndiyo  kwanza  naliskia hapa, " alisema.

Katika kikao hicho wakurugenzi wa  halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waliwasilisha maombi ya bajeti maalumu za maeneo yao.   

Suala hilo lilimshangaza Mongella na kulazimika kutafuta uzoefu kwa kuwahoji wakurugenzi wazoefu  waliohudhuria kikao hicho.

Wakurugenzi hao walisema kwa uzoefu walio nao  maombi ya bajeti maalumu  hayatakiwi kuzidi Sh milioni 700  au Sh bilioni 1. 5.

Walisema  bajeti iliyowahi kuzidi kiwango hicho ni ile iliyotolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa na hiyo ilitokana na halmashauri hiyo kuwa mpya.

  Mongella aliagiza hoja hiyo ifutwe hadi atakapokutana na wakurugenzi hao na kuijadili kwa vile  kiasi cha fedha kinachoombwa na halmashauri zote kinazidi makusanyo ya ndani  ya mkoa mzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles