RC aagiza wananchi kurudishiwa fedha walizochanga kwaajili ya ujenzi wa visima

0
569

Amina Omari, Muheza

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, ametoa wiki  tatu kwa Halimashauri ya Wilaya ya Muheza kurudisha fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kuchimba visima ili kumaliza kero ya uhaba wa maji vijijini.

Ametoa agizo hilo leo Jumamosi Agosti 10, wakati wa ziara yake ya kata kwa kata wilayani humo kusikiliza kero za wananchi.

Amesema kuwa fedha hizo zimechangishwa kwa kipindi cha miaka mitatu bila miradi kutekelezwa.

“Naagiza Halimashauri rudisheni fedha za wananchi ambazo kila kata mmechangisha laki tano na Kama mmezitumia mtazitapika” amesema.

Halimashauri ya Muheza iliingia mkataba na muwekezaji kwa ajili ya kuchimba visima katika vijiji kwa gharama ya sh. laki tano miradi ambayo haijaweza kutekelezwa hadi sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here