28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RC AAGIZA WAAJIRI BINAFSI KUTOA MIKATABA YA AJIRA

Na SAM BAHARI

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Talack, ameagiza waajiri wa sekta binafsi kuhakikisha wanatoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao.

Alivitaka vyama vya wafanyakazi kusimamia jambo hilo  kutasaidia kuongeza tija ya utendaji wa kazi.

Alikuwa akizungumza juzi na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Shinyanga.

Talack alisema amebaini  sehemu kubwa ya wafanyakazi walioajiriwa na sekta binafsi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya kutokuwa na mikataba ya ajira jambo ambalo limekuwa likishusha ufanisi wao kazini.

Alisema wapo baadhi ya waajiri ambao wamekuwa wakitoa mikataba kwa wafanyakazi lakini wamekuwa wakiwazuia   kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

RC alisema wengine wamekuwa wakiwatishia kuwafukuza kazi iwapo watajiunga na vyama hivyo hivyo kuwaonya   wenye tabia hiyo kwa kuwa ni kinyume na sheria za kazi.

Alisema serikali itaingilia kati suala la waajiri wakorofi wa sekta binafsi ambao hushindwa kufuata sheria za nchi hususan sheria ya ajira na uhusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 na kutowapatia mikataba wafanyakazi wao.

“Wapo waajiri ambao wamekuwa na tabia ya kutotoa hati za malipo ya mishahara ya wafanyakazi wao, pia hawazingatii saa za kazi wala hawawalipi posho za muda wa ziada, hawalipi michango katika mifuko ya jamii.

“Sasa ninyi vyama vya wafanyakazi mnapaswa kulikema hili pia,” alisema.

Alisema changamoto nyingine ni kwamba waajiri wa sekta binafsi hawatoi vitendea kazi vinavyolingana na mahitaji ya kazi kwa wafanyakazi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles