29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

RAY C UNA DENI KUBWA KWA MASHABIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

AMEJIZOLEA umaarufu mkubwa kwenye Bongo Fleva kutokana na tungo zake za mapenzi, Rehema Chalamila ‘Ray C’ au kiuno bila mfupa, amerejea tena ulingoni tayari kurudisha heshima yake iliyopotea kutokana na matatizo ambayo nisingependa kuyazungumza hapa.

Sipendi kuyazungumza hapa kwa kuwa huu ni wakati wetu wa kusherehekea ushindi wa shujaa Ray C, aliyeweza kupigani vita nzito iliyowamaliza vijana wengi wa Tanzania.

Ray C alikonga nyoyo za mashabiki kwa nyimbo kali zenye kuleta hisia za mapenzi, usanii wake uliojaa kipaji kikubwa ulipotiwa kwenye utunzi wa mashairi kisha sauti yake yenye msisimko wa mahaba ikapita kwenye midundo ya mapenzi zikazaliwa nyimbo kubwa kama Mapenzi Matamu, Na Wewe Milele, Uko Wapi na nyinginezo nyingi.

Hata alipopata wasaa wa kufanya kava za nyimbo za wanamuziki wa zamani, Ray C alifanya vyema kiasi kwamba kwa watu wasiofahamu wanaweza kusema ni wimbo wake, sikiliza Mahaba ya Dhati ya Bi Mwanahela utabaini kipaji cha mrembo huyu.

Baada ya misukosuko yote, Ray C amerudi kwa kishindo kwenye Bongo Fleva, hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya unaoitwa Unanimaliza, uliotengenezwa na mtayarishaji muziki, Abby Dady.

Huu ni wimbo uliomrudisha kwa kishindo kwenye muziki na safari hii akiwa chini ya uongozi wa tovuti ya wasafi.com, ambayo imechukua jukumu la kumsimamia ili aweze kulipa deni analodaiwa na mashabiki.

Amekuja kufanya muziki kibiashara, tayari ameweka saini ya kuuza muziki wake kwenye tovuti hiyo ambayo inamilikiwa na msanii mwenzake, Diamond Platnumz, hivi sasa ni kazi juu ya kazi kama anavyodai yeye mwenyewe.

Mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa mashabiki ni ishara ya ukubwa wa deni analodaiwa. Nadhani huu ni muda wake mwafaka wa kulipa na sina shaka naye, kwani yupo tayari kuwapa mashabiki kile walichokikosa muda mrefu alipokuwa matatizoni.

Ili alilipe deni analodaiwa na mashabiki, anahitaji sana msaada wetu wa kusapoti kazi zake. Tukiweza kumuunga mkono katika uamuzi wake wa kuamua kufanya biashara ya muziki, naamini Ray C atakuwa balozi mzuri kwa vijana wengine walioko kwenye majanga kama alivyokuwa yeye kuwa wanaweza kutoka huko na kuwa watu safi mbele ya jamii.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles