Ratiba Bongo Star Search 2019 yaanza na Arusha

0
1019

Brighiter Masaki

MSIMU mpya wa Bongo Star Search, kumtafuta muimbaji mahiri, usaili umeanza Leo, kusaka vipaji jijini Arusha, na kufatiwa na mikoa mitano hapa Tanzania.

Akizungumzia Pendo Mango, amesema Usahili umeanza jijini Arusha eneo la Fuzz-Pointzone Resort (Mianzini) na utaendelea hadi September 29.

“Tarehe 4 na 5 Oktoba kutakuwani Mwanza Rock City Mall, 10 na 11 ya mwezi huo huo ikifanyika Mbeya eneo Mbeya City Pub & Lounge wakati tarehe 17 na 18 itakuwa Dodoma mahala Royal Village Hotel na kwa jiji la Dar es salaam itakuwa tarehe 23, 24 na 25 katika eneo la National Museum”anasema.

Aidha aliongezea kwa kusema kuwa ” Watazamaji pia watashiriki kwenye mashindano na kumchagua mshindi kwa kupiga kura mtandaoni, Bongo Star Search inawakaribisha wale wote wenye vipaji kushiriki usaili kwenye Mikoa husika na kwenye Mtandao kupitia App.”

” Watakaotoa kura za ndio au hapana kwa washiriki baada ya kuangalia umahiri wao katika kuimba, Na ukipata kura tatu za ndio moja kwa moja utakua umeshinda kuingia mchuano wa pili.” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here