Chicago, Marekani
Soko la muziki la Afrika Mashariki limeendelea kuwa kivutio kwa wasanii wa Ughaibuni na sasa hutumia njia mbalimbali ili waweze kupata nafasi ya kusikilizwa mamilioni ya mashabiki.
Kutana na Rastabwoykell, mwanamuziki wa Reggae na Hip hop anayeamini katika imani ya Rastafari anayeishi Chicago Illinois nchini Marekani.
SWALI: Rastabwoykell ni nani na uliingia vipi kwenye muziki?
Rastabwoykell: Mimi ni rapa, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki kutoka hapa Chicago, IL ambaye nachanganya ladha vitu vya Hip hop na Reggae.
Nilikuwa naongoza video za muziki lakini baada ya Polisi wa Chicago kuiba kamera na vifaa vingine nilichokuwa nimebaki nacho ni studio tu hapo nikajiongeza kwa kuwa msanii ninayejitegemea na ninashukuru mpaka sasa nafanya vizuri.
SWALI: Changamoto zipi unakutana nazo kwenye harakati zako za muziki?
Rastabwoykell: Ninakabiliwa na changamoto nyingi hasa kutoa muziki wangu nje kwa sababu umekuwa ni biashara kubwa ila tatizo mitandao ya Facebook na YouTube imekuwa ikijaribu kunizuia kutangaza nyimbo zangu kama ule unaoitwa kama Egypt.
SWALI: Wasanii gani Afrika Mashariki unatamani kufanya nao kazi?
Rastabwoykell: Sina msanii maalum lakini ningependa kushirikiana na wote wanaofanya vizuri pande hizo.
SWALI: Rastabwoykell ni nani na uliingia vipi kwenye muziki?
Rastabwoykell: Mimi ni rapa, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki kutoka hapa Chicago, IL ambaye nachanganya ladha na vitu vya Hip hop na Reggae.
Nilikuwa naongoza video za muziki (video director) lakini baada ya Polisi wa Chicago kuiba kamera na vifaa vingine nilichokuwa nimebaki nacho ni studio tu hapo nikajiongeza kwa kuwa msanii ninayejitegemea na ninashukuru Jah mpaka sasa nafanya vizuri.
SWALI: Mafanikio gani umeyapata mpaka sasa?
Rastabwoykell: Mafanikio ni mengi kama hivi nilifaulu kutoka kuwa mpiga picha wa video kwenda kuwa msanii, mtayarishaji wa muziki niliyeanzisha lebo yangu mwaka huu.
SWALI: Nje ya sanaa unapenda kufanya nini?
Rastabwoykell: Nje ya muziki wakati mwingi mimi hupanga na kufikiria mikakati mipya na kutafiti aina fulani ya habari ambazo zinaweza kuhamasisha wazo jipya.
SWALI: Ujumbe gani ulitaka uwafikie watu kupitia santuli yako ya ‘The Mystic Sound of Rastabwoykell’?
Rastabwoykell: Ujumbe niliotaka uwafikie watu ni kuiga kadiri uwezavyo mfano mzuri ambao uliwekwa na Kristo sio kwa kuhubiri tu bali kwa kutafuta njia yako mwenyewe.
Muziki wangu wote unaweza kupatikana kwenye wavuti yangu ya www.RastaBwoyproductions.com/music
Ninafanya kazi kwenye albamu nyingine hivi sasa ambayo iliongozwa na mwalimu wangu wa ngoma anaitwa Papa Mangue na nina mpango wa kubadilisha mfumo wa muziki ili niweze kuwafikia watu wengi sana.