30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RAS AAGIZA WAGONJWA WANAUME WAFANYIWE TOHARA

Na ABDALLAH AMIRI-IGUNGA

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora (RAS), Dk. Thea Ntala amewaagiza waganga wakuu wa wilaya zote za mkoa wake kuhakikisha wanasimamia suala zima la tohara kwa baadhi ya watu watakaobainika hawajafanyiwa tohara pindi wanapokwenda kutibiwa hospitali.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kilichofanyika Februari 2, mwaka huu, Dk. Ntala alisema hali inaonesha kuwa wapo wananchi wengi na watu wazima mbao hawajafanyiwa tohara hali ambayo imekuwa ikiwasababishia maambukizi ya magonjwa.

“Kila atakayekwenda kutibiwa hospitalini ikibainika kuwa hajawahi kufanyiwa tohara, hata kama anaumwa kichwa mfanyieni hapo hapo wakati akitibiwa kichwa,” aliagiza.

Aidha aliwataka madiwani wa halmashauri zote Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanatenga fedha kila mwaka zitakazosaidia kununua pikipiki kwa ajli ya maofisa kilimo ili waweze kuwa na usafiri wa uhakika wa kusimamia kilimo.

Dk. Ntala alisema kumekuwa na upungufu wa pikipiki kwa maofisa kilimo hali ambayo imekuwa ikisababisha wakulima wengi kutofikiwa na maofisa kilimo hivyo alisema katika mpango wa muda mrefu wanapaswa kuanza kutenga fedha katika bajeti zao ambazo wanaweza kuzitumia kwa ajili ya kununulia pikipiki kwa kila kata.

Wakichangia hoja katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Isakamaliwa, Dotto Kwilasa (CCM) pamoja na Lucas Bugota wa Kata ya Mbutu (CCM) walimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Revocatus Kuuli kuwakamata na kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi wa Kata ya Choma wanaotuhumiwa kula fedha za manunuzi ya mashine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles