31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rani Sanitary Pads yaongeza mzuka Tanzanite

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WASAMBAZAJI wa taulo za kike aina ya Rani Sanitary Pads, wametoa taulo hizo kwa wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya wasichana wenye umri chini ya miaka 20,Tanzanite ikiwa ni kuongeza hamasa kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la dhidi Ethiopia.

Mchezo huo utapigwa kesho Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar ambako kikosi hicho kimeweka kambi tangu wiki iliyopita kujiandaa na mechi hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi taulo hizo, muwakilishi wa Rani Sanitary Pads, Mawi Zahor kambini Zanzibar jana Januari 21,2022, amesema wameamua kufanya hiyo ili kuwapa hamasa kwa wachezaji ili timu iingie uwajani ikiwa inajiamini.

Mawi amesema anaamini Tanzanite itashinda mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri na kambi tulivu waliyoipata.

“Tumekuwa wadau wakubwa wa soka la Wanawake nchini, ndiyo maana tumeona tuje hadi huku Zanzibar kuungana na hawa vijana wetu katika maandalizi ya mchezo huo wa Jumapili.

“Tunaamini kwa tulichokitoa kitakuwa kizuri maana timu ya taifa inatakiwa kutumia taulo ambazo ni bora,” Mawi.

Rani Sanitary Pads ambao ni mdhamini mweza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, wamekuwa na utaratibu wa kutoa taulo hizo kwa kikosi hicho na vikosi mbalimbali za timu ya Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles