30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

RAMSEY: MITANDAO YA KIJAMII HAINA MAANA KWANGU

LAGOS, NIGERIA


STAA wa filamu nchini Nigeria, Ramsey Nouah, ameweka wazi sababu za kutojihusisha na mitandao ya kijamii kama ilivyo kwa mastaa mbalimbali duniani.

Mkali huyo wa filamu amesisitiza kwamba, haoni sababu ya kuwa kwenye mitandao ya kijamii wakati kazi zake zinaenda vizuri bila ya mitandao.

“Sidhani kama mitandao ya kijamii itanifanya niongeze mafanikio yangu, lakini ninaamini ubora wa kazi zangu unaweza kufika kwa kila mmoja ambaye anatumia mitandao, lakini si lazima na mimi nitumie mitandao.

“Muda wangu mwingi nautumia kwa ajili ya kufanya mambo yangu na wale ambao wanataka kufanya kazi na mimi bado wananipata kwa urahisi bila ya kujali kwamba sipo kwenye mitandao kama ilivyo kwa wengine,” alisema staa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles