25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Ramaphosa: Tusiruhusu vita vya niaba barani Afrika

Addis Ababa, Ethiopia

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, Waafrika hawapaswi kuruhusu bara lao liwe medani ya vita vinavyopiganwa kwa niaba ya pande nyingine.

Rais Ramaphosa aliyasema hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika mjini Addis Ababa na kuongeza kuwa, Waafrika hawapasi kuwaruhusu wageni kuwasha moto wa vita na mizozo barani mwao na kuzitumbukiza nchi za bara hilo katika vita vya niaba.

“Waafrika wote wanawajibika kutengeneza amani na ustawi kwa ajili ya Afrika,” alisema Ramaphosa.

Rais Ramaphosa ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika alizitaka nchi zote za bara hilo kusimama kidete kwa ajili ya kukabiliana na njama zinazotaka kulitumbukiza bara hilo katika mapigano na vita vya ndani.

Alikutaja kukomesha machafuko nchini Libya na kukamilisha makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini kuwa ndiyo malengo mawili muhimu zaidi ya kipindi chake kama mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika.

Mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika ulianza kazi zake Jumapili katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ukijadali masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Libya, mpango wa Donald Trump wa “Muamala wa Karne” kuhusu Palestina na suala la kuondolewa Sudan katika orodha ya magaidi ya Marekani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles