31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ramaphosa: Mlipuko wa virusi vya corona utakuwa mbaya zaidi

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametehadharisha kuwa hali ya mlipuko wa virusi vya corona inaelekea kuwa mbaya zaidi, wakati akitangaza kulegeza masharti ya kubaki nyumbani.

Rais Ramaphosa alisema ana kuwa zaidi ya watu 22,000 wamerekodiwa kuwa na maambukizi juma lililopita.

Pamoja na hayo, alisema kuwa sharti la kutotoka nje halijaondolewa moja kwa moja.

Alitangaza kuwa kuanzia Juni 1 mwaka huu, masharti zaidi yataondolewa.

Rais Ramaphosa alikuwa akizugumza baada ya kampuni ya madini nchini Afrika Kusini kusema kuwa wafanyakazi 164 katika mgodi wa dhahabu karibu na ji wa Johannesburg wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Nchi hiyo imethibitisha vifo vya watu 429 mpaka sasa kutokana na Covid-19.

Sharti la muda wa kurejea nyumbani halitakuwepo tena, biashara zaidi zitaruhusiwa kuendelea na shule zitafunguliwa, Rais Ramaphosa alieleza.

Marufuku ya biashara ya pombe itaondolewa kwa idadi maalumu ya mauzo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee na “kwa masharti ya siku maalumu na saa maalumu”, alieleza kiongozi huyo.

Lakini  Ramaphosa alisema marufuku ya biashara ya sigara itaendelea kuwepo “kutokana na hatari za kiafya zinazotokana na uvutaji wa sigara”.

Pia alisema shule zitafunguliwa kwa awamu kwa sababu wanazingatia maendeleo ya watoto na kizazi chote cha watu wanaojifunza hawapaswi kuwa waathirika wa kudumu wa janga hili.

Lakini alisema kuwa hakuna mzazi atakayeshurutishwa kumpeleka mtoto shuleni kama watakuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao shuleni.

ALICHOSEMA KUHUSU KUENEA KWA VIRUSI?

Rais Ramaphosa amekuwa kwenye shinikizo kubwa akitakiwa kulegeza masharti ili kuufungua tena uchumi.

Hatahivyo, ameutahadharisha Umma kuwa hali itakuwa mbaya siku za usoni.

“Tutarajie kuwa idadi ya watu walioambukizwa itaongezeka zaidi na kwa haraka. Janga la corona nchini Afrika Kusini litakuwa baya zaidi kabla ya hali kuwa nzuri,” aliongeza.

Kuna uwezekano wa takriban watu 40,000 kupoteza maisha nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka, wanasayansi walitahadharisha juma lililopita.

KINACHOENDELEA KATIKA MGODI WA MPONENG

Mgodi wa Mponeng ni mgodi mrefu zaidi kwenda chini kuliko mgodi mwingine wowote duniani.

Operesheni zake ziliathiriwa baada ya watu 164 kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Wengi kati ya waliobainika walikuwa hawaoneshi dalili zozote za kuwa na virusi hivyo.

Wote wametengwa, kwa mujibu wa wamiliki wa mgodi, AngloGold Ashanti.

HALIILIVYO ETHIOPIA

Huko Ethiopia imethibitisha kugunduliwa wagonjwa wengine 88 wa Covid-19 na kufanya idadi ya kesi za corona zilizogunduliwa nchini humo hadi jana Jumatatu asubuhi kufikia 582. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana na Wizara ya Afya ya Ethiopia.

Hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kugunduliwa kwa siku moja katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ambapo juzi Jumamosi ilitangaza kugundua wagonjwa 61 wa Covid-19.

Wizara ya Afya ya Ethiopia ilisema, wagonjwa wote 88 wa corona waliothibitishwa jana Jumapili ni raia wa Ethiopia. 51 kati yao ni wanaume na 37 ni wanawake na umri wao ni baina ya miaka minane hadi 75.

Wizara hiyo aidha ilisisitiza kuwa, kati ya wagonjwa hao 88 wa Covid-19, 13 wamewahi kusafiri nje ya Ethiopia, 20 walikuwa na mawasiliano na wagonjwa wa corona wanaojulikana na 55 waliobakia hawajawahi kusafiri nje ya Ethiopia na wala hawajawahi kuwa na mawasiliano na wagonjwa wanaojulikana wa corona.

Siku ya Jumapili, Mei 24, 2020 Ethiopia iligundua wagonjwa wapya 88 wa corona

Wizara ya Afya ya Shirikisho la Ethiopia pia ilisema, hadi hivi sasa wagonjwa 152 wa Covid-19 wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani. Huko nyuma wizara hiyo iliwahi kuthibitisha kuwa watu watano wamefariki dunia kwa corona nchini humo. 

Ethiopia ni nchi ya pili yenye watu wengi barani Afrika. Ina watu milioni 107. Kesi ya kwanza ya corona ilithibitishwa Machi 13 mwaka huu nchini humo.

Serikali ya Ethiopia imeweka sheria nyingi na kali za kupambana na maambukizi ya corona hasa kwa vile nchi hiyo ni Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) na inapokea wageni wengi.

BBC, AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles