23.9 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

RAIS ZAMBIA AMPONGEZA MWAMUZI URUSI

LUSAKA, ZAMBIA


RAIS wa nchi ya Zambia, Edgar Lungu, amesema anavutiwa na utendaji kazi wa mwamuzi wa soka wa Zambia, Janny Sikazwe, katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi.

Lungu alisema Sikazwe anawakilisha Zambia vizuri kwa  kuonyesha kiwango cha kipekee na anatarajia ataendelea na utendaji huo.

Kauli hiyo ya Lungu aliitoa juzi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda (KKIA) kabla ya kuelekea nchini Uturuki.

Rais  huyo pia aliwahimiza  waamuzi wa nchi hiyo kuiga mafanikio ya Sikazwe.

“Sikazwe anafanya kazi nzuri, tulimwona, tunamtakia kila la kheri katika maisha yake ya uamuzi,” alisema Lungu na kuongeza:

“Msimwangushe, watu wanatakiwa kuhamasika kutokana na kazi yake”.

Rais huyo alisema kutokana na kazi nzuri anayofanya Sikazwe katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, anaweza kusaidia katika maendeleo ya sekta nyingine nchini humo inayohusiana na uamuzi na mchezo wa soka.

Sikazwe ni mmoja kati ya waamuzi wawili wa Afrika waliomo katika orodha ya waamuzi 17 waliotangazwa kuendelea kuisimamia michuano ya Kombe la Dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles