23.6 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Yanga aahidi kubakiza wachezaji wote wakali

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa likizo ya mwezi mmoja kwa wachezaji wake, huku ikiahidi kufanya usajili mkubwa kuimarisha kikosi hicho na kumbakiza kila mchezaji wanayemta kwa msimu ujao.

Hayo yamesemwa na Rais wa klabu hiyo, Hersi Saidi leo Juni 5, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa pamoja na kupata mafanikio makubwa msimu huu, wanajipanga kufanya vizuri zaidi msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na michuano mingine.

Ameeleza kuwa mafanikio ya msimu huu yametokana na kujitoa kwa dhati kwa wachezaji wao na uongozi mzima wa benchi la ufundi.

“Niwapongeze wachezaji wetu, kazi kubwa mmeifanya, Kuanzia leo tunawapa wachezaji wetu likizo ya mwezi mmoja, tutakutana nao tena mwanzoni mwa mwezi wa saba wa kujiandaa na msimu mpya ambapo tutakuwa tayari tumefanya usajili wa kuimarisha kikosi chetu,” amesema Hersi.

Msimu huu Yanga imefanikiwa kutetea mataji yake mawili la Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la TFF, huku michuano ya Kimataifa ikifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles