27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais, Waziri Mkuu wakamatwa Burkina Faso

kafando1OUAGADOUGOU, BURKINA FASO

WALINZI wa Ikulu nchini Burkina Faso wamemkamata Rais wa mpito, Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida muda mchache tu baada ya jeshi kuivunjilia mbali serikali ya mpito.

Hatua hiyo ya jeshi imeitumbukiza nchi katika hali ya wasiwasi ikiwa ni wiki chache tu kabla uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani, Blaise Compaore.

Kukamatwa kwao kulisababisha maandamano barabarani hadi nje ya Ikulu, ambako viongozi hao walikuwa wakizuiliwa.

Milio ya risasi ilisikika wakati wanajeshi walipokuwa wakiwatawanya mamia ya waandamanaji wenye hasira.

Inaaminika walinzi hao wa Ikulu pamoja na baadhi ya wanajeshi wanamtii Campaore, ambaye aling’olewa Oktoba mwaka jana kwa maandamano baada ya kujaribu kuchakachua katiba ili aendelee kuongoza.

Kafando na Luteni Kanali Zida walipewa jukumu la kuandaa uchaguzi mpya wa urais mwezi ujao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon ameghadhabishwa na hatua hiyo na kutaka viongozi hao waachiwe mara moja, akisema inakiuka Katiba ya Burkina Faso na mkataba wa utawala wa mpito.

Marekani imelaani vikali juhudi yoyote ya kuchukua madaraka kupitia njia zilizo nje ya katiba au kuisuluhisha mivutano ya kisiasa kutumia nguvu.

“Tumeweka Baraza la Taifa la Demokrasia litakalopanga uchaguzi wa kidemokrasia,” alisema afisa mmoja aliyevaa sare za kijeshi ambaye hakutambulika.

Rais Kafando na Zida walizuiliwa katika mkutano wa mawaziri katika makao ya rais katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Hatua hiyo inajiri siku mbili tu baada ya Tume ya Uchaguzi kutoa agizo la kuvunjiliwa mbali kwa Kikosi cha Walinzi wa Rais (RSP).

Hakuna majeruhi walioripotiwa lakini kumedaiwa kuwepo kwa hali ya wasiwasi huku maduka yakifunga biashara mapema na raia wengi kuelekea majumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles