26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Zimbabwe amtumia JPM ujumbe

Mwandishi wetu-Dar es Salaam

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ambaye ni Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji, Mazingira na Makazi Vijijini, Pretence Shiri.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Shiri amekabidhi barua kutoka kwa Rais wa Mnangagwa.

 Shiri ameishukuru Tanzania kwa mchango ilioutoa kwa Zimbabwe wakati wa kupigania uhuru uliopatikana mwaka 1980, na amebainisha kuwa Wazimbabwe wanaichukulia Tanzania kuwa ni nyumbani.

“Tunafurahi sana kuwa hapa Tanzania, tunajisikia ni nyumbani kwetu, bila Tanzania Zimbabwe isingepata uhuru mwaka 1980, ingechukua muda mrefu sana, lakini tunafurahi kuwa Watanzania walijitolea kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Zimbabwe inakuwa nchi huru” alisema Shiri.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Jumuiya ya Ulaya, Charles Stuart na baada ya mazungumzo hayo Stuart amesema mazungumzo baina yao yalikuwa mazuri na yamehusu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Umoja wa Ulaya na dhamira ya umoja huo kuisadia Tanzania.

Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umekuwa imara siku zote, na kumekuwa na maeneo mengi ya uhusiano yenye maslahi muhimu kwa pande zote na kwa miaka mingi alisema Stuart.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles