30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA ZAMANI BRAZIL KWENDA JELA

BRASILIA, BRAZIL


MAHAKAMA ya juu ya Brazil jana imekataa ombi la Rais wa zamani wa nchi hii, Luiz Inacio Lula da Silva kukaa nje ya gereza wakati akisubiri uamuzi wa rufaa yake ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 12 kwa mashtaka ya rushwa.

Uamuzi huu huenda ukahitimisha maisha ya kisiasa ya Lula, ambaye anaongoza kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

Lula alikuwa na matumaini ya kuruhusiwa kukaa nje ya gereza wakati akisubiri rufaa yake kupinga hukumu hiyo isikilizwe ili kumrahisishia harakati zake za kurudi Ikulu.

Baada ya saa 10, majaji 11 wanaosikiliza shauri hilo walipiga kura, sita walikataa ombi lake hilo huku watano wakiliunga mkono.

Lula ambaye anapendwa na wabrazil wengi atakosa sifa ya kuwania urais katika uchaguzi ujao iwapo hukumu hiyo haitabatilishwa.

Hukumu hiyo imetokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata ya ufisadi, inayojulikana kama ‘Operation Car Wash’.

llibainika kuwa Lula alikula rushwa ya Euro 790,000 sawa na Sh bilioni 1.6 mwaka 2014.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles