Rais wa Valencia atishiwa kifo

0
602

VALENCIA, HISPANIA

UONGOZI watimu ya Valencia, umepeleka taarifa polisi ya rais wao Anil Murthy kutishiwa kuuawa na watu wasiojulikana.

Tishio hilo lilitokea mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Deportivo Alaves mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania.

Katika mchezo huo mashabiki walionekana kuwa na vurugu wakidai kutoridhishwa na aina ya uchezaji wao japokuwa walipata matokeo mazuri.

Murthy pamoja na mmiliki wa timu hiyo Peter Lim, wamekuwa wakishambuliwa na mashabiki kutokana na maamuzi yao ya kumfukuza kocha Marcelino Toral, Septemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Albert Celades.

“Idara ya sheria ya klabu ya Valencia, imewapa polisi ushahidi wa vitisho vikali ikiwa pamoja na vitisho vya kifo vilivyotumwa na watu wasiojulikana kwenda moja kwa moja kwenye simu ya rais wa timu saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Alves, vitisho kama hivi vinaathari kubwa sana,” waliandika kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya timu hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mchezo huo, mashabiki walionekana nje ya uwanja wao wakiwa kwa wingi na mabango ambayo yanamtaka rais huyo kuhakikisha anaiongoza timu tofauti na vile anavyojiongoza yeye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here