28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Sudan Kusini apiga marufuku wimbo wa Taifa kuimbwa bila uwepo wake

Juba, Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amepiga marufuku  wimbo wa taifa kuimbwa katika hafla ambazo hayupo kwa maelezo kuwa  wimbo huo ni maalum kwa ajili ya Rais ambapo amesema wenye ruhusa ya kuimba wimbo wa taifa akiwa hayupo ni Balozi za nchi hiyo na shule pekee.

Rais Kiir alitoa agizo hilo Ijumaa Julai 19 wakati wa kikao chake na Baraza la Mawaziri.

Katika mahojiano yake na Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei amesema agizo hilo limetokana na viongozi wa serikali na taasis mbalimbali kuimba wimbo wa taifa bila mpangilio hivyo ni matumizi mabaya ya wimbo huo uliotungwa kabla  ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 2011.

“Kwa taarifa tu kila mmoja ajue wimbo wa taifa ni maalumu kwa ajili ya Rais tu na unapaswa kuimbwa katika hafla ambazo zimehudhuriwa na Rais tu na sio kwa kila mtu.

“Tunaona hivi sasa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Magavana  na Wakuu wa Mikoa wakiwepo kwenye hafla mbalimbali wimbo huu unaimbwa,” Makue aliieleza AFP.

Waziri huyo japo hakuweka wazi adhabu itakayotolewa kwa mtu akayekiuka agizo hilo aliongeza na kusema: “Hili ni agizo la Rais na usipotii agizo la Rais utabeba msalaba wako mwenyewe.”

Makue pia amesema viongozi wa jeshi wamezuiwa kuhutubia umma wakiwa katika mavazi ya kijeshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles