26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Rais wa Poland aambukizwa virusi vya corona

WARSAW, POLAND

WAKATI Marekani na nchi nyingine zikiendelea kushuhudia maambukizi ya juu ya virusi  vya corona, Rais wa Poland, Andrzej Duda ameambukizwa virusi vya hivyo, kulingana na taarifa zilizotolewa jana na msemaji wake baada ya kufanyiwa vipimo. 

Msemaji huyo, Blazej Spychalski, ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba Duda amewekwa karantini na anaendelea vizuri. 

Duda amepata virusi hivyo katika wakati ambapo kunashuhudiwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini mwake. 

Ongezeko hilo la viwango vya maambukizi linatajwa kuuathiri mfumo wa afya nchini humo. Madaktari wanasema wagonjwa wanakufa sio tu kutokana na COVID-19, bali pia kutokana na magonjwa mengine ambayo hospitali zilizozidiwa zinashindwa kuwatibu. 

Serikali ya Poland jana ilitangaza vikwazo vipya, ikijaribu kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles