24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Msumbiji ataka uhusiano wa uchumi

Pg 2Na Debora Sanja, Dodoma
RAIS wa Msumbiji, Filipe Nyussi ametaka uhusiano wa nchi yake na Tanzania ulenge pia katika sekta ya uchumi.
Nyusi alitoa kauli hiyo Dodoma jana wakati akihutubia Bunge ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza nchini tangu alipochaguliwa kuongoza Msumbiji.
Uhusiano huu usiishie kwenye siasa, usaidie pia watu kusafiri ndani ya nchi hizi kwa urahisi… sisi nchini kwetu tutaruhusu Watanzania waje kwa urahisi zaidi na wanapokuja wakae muda mrefu bila shida yoyote.
“Tungependa pia waje Msumbiji kufanya biashara wawasaidie pia watu wa nchini kwangu, kwa hiyo mbali na siasa tungepena kuekeleza uhusiano wetu katika sekta ya uchumi, utalii na elimu,” alisema.
Alitaka raia wa nchi hizo mbili waishi kwa amani na kunufaika na uhusiano huo.
“Tulinde nchi zetu hizo mbili kwa kupigana vita dhidi ya ufisadi na ugaidi, vita ambayo dunia nzima inapigana nayo,” alisema Rais Nyussi.
Alisema amefurahi kupata fursa ya kutembelea Tanzania na kulihutubia Bunge pamoja na kujifunza jinsi Bunge la Tanzania linavyofanya kazi ikiwamo jinsi ya kuendeleza demokrasia.
“Bunge la Msumbiji linafanya kazi yake ikiwamo kutoa uamuzi mbalimbali wa Serikali, tunafanya kazi kwa pamoja ya kupiga vita ufisadi na sasa tuna kazi ya kuandaa bajeti,” alisema.
Alisema Msumbiji imekuwa na uhusiano mzuri tangu kabla ya Uhuru, uhusiano ulioasisiwa na Hayati Samora Machael na Mwalimu Nyerere.
Alisema yuko Tanzania kuendeleza urafiki huo na kujifunza jinsi ya kuendeleza demokrasia.
Akitoa salamu za shukrani, Spika wa Bunge, Anne Makinda mbali na kumpongeza Rais Nyussi kwa kuchaguliwa kuiongoza Msumbiji alisema Rais huyo ameweka historia kwa kuwa Raia wa kwanza wa Msumbiji kulihutubia Bunge la Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles