24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Malawi ziarani kwa siku tatu nchini

Na BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi, amesema leo, kutakuwa na ugeni wa ujio wa Rais wa Jamuhuri ya Malawi, Dk Lazarus Chakwera ambaye atakuwa na ziara ya siku tatu  Oktoba 7 hadi 9.

Alisema Rais wa Malawi Prof Chakwera atafanya ziara ya kitaifa hapa nchini ya siku 3 kuanzia Oktoba 7 hadi 9 mwaka huu na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,  Prof Kabudi alisema kuwa hii itakuwa ziara rasmi ya kitaifa ya Kwanza kwa Chakwera tangu aingie madarakani Juni 2020.Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi mbili na kuendelea kuimarisha ujirani mwema uliopo.

“Itakumbukwa Aprili 24,25 2019 Dkt Magufuli alifanya ziara rasmi nchini Malawi, na Julai 6, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, alishiriki uzinduzi rasmi wa Chakwera ambaye ni Rais wa sita wa Malawi.”alisema Prof Kabudi

Aidha alisema kuwa Rais wa Malawi Dkt Chakwera atawasili hapa nchini Oktoba 7 na atapokelewa na mwenyeji wake, baada ya mapokezi hayo ya kitaifa mgeni wetu ataendelea na ratiba zingine zitakazokuwa zimepangwa kwa siku hiyo.

“Dkt Chakwera atapata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam, ili kujionea shughuli mbalimbali za bandari na uboreshaji wa miundo mbinu ya bandari, Uboreshaji wa miundombinu utaharakisha utoaji wa mizigo bandarini na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora bandarini.”alisema Prof Kabudi

Alisema kubwa akiwa bandarini atatembelea kituo cha kuhifadhia mizigo cha Malawi (Malawi Cargo Centre) ambacho kimekuwa alama muhimu ya ushirikiano wa Malawi na Tanzania.

“Wakati wa ziara hiyo Dkt Chakwera akiwa na Rais Magufuli wataweka jiwe la msingi katika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam, ishara ya ushirikiano wetu na umoja katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Ushirikiano wa Tanzania na Malawi ni mzuri na unaendelea kuimarika siku hadi siku, nchi hizi mbili zimeendelea kushirikiana katika nyanja za kisiasa, ulinzi na usalama, kiuchumi, kijamii, na yale ya kikanda hususa ndani ya jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika. 

Aidha aliongeza nchi hizi zimendelea kushirikiana katika miradi ya pamoja ikiwemo ujenzi wa kituo cha kutoa huduma cha pamoja mpakani (OSBP) katika mpaka wa Songwe, Kasumulo pamoja na miladi ya bonde la mto Songwe, miradi yote ipo katika hatua za utekelezaji.

“Vilevile nchi zetu zimeendelea kushirikiana kuboresha miundombinu katika ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor) Serikali ya Malawi imeendelea kuimarisha miundombinu ya barabara inayofika bandari ya Nkhata Bay hatua kama hiyo imeendelea kuchukuliwa na serikali yetu kuimarisha miundombinu ya barabara kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay.

“Nchi ya Malawi ni miongoni mwa nchi zenye uwekezaji hapa nchini, uwekezaji kutoka nchini Malawi umejikita katika sekta ya fedha, uzalishaji na usafirishaji, ujenzi, kilimo na mafuta, takwimu za kituo cha uwekezaji tanzania (TIC),

Septemba 2020 zinaonyesha kuna jumla ya miladi 8 kutoka Malawi iliyosajiliwa na kituo hicho ambayo inajumla ya thamani ya Dora za Marekani Bilioni 30.11 na imetoa ajira kwa watanzania 390.

Alisema pia baadhi ya kampuni kutoka Tanzania zimeweza kuwekeza na kuuza bidhaa zao nchini Malawi zikiwemo kampuni za Mohamed Enterprises, Barkhesa Group, SIMSO Company Ltd, Mount Menu Group, pamoja na makampuni mengine mengi yakiwemo ya usafirishaji wa mafuta.

“Ushirikiano wa biashara kati ya Tanzania na Malawi, takwimu kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwango cha bidhaa ambazo Tanzania imesafirisha kwenda Malawi kimezidi kuongezeka toka Sh Bilioni 111,082.70 mwaka 2015 hadi kufikia Sh Bilioni 130,758.10 mwaka 2019.

“Kiwango cha biashara ambacho Tanzania kimeingiza kutoka Malawi kimeongezeka kutoka Sh Bilioni 26,999.05 kwa mwaka 2015 hadi kufika Sh Bilioni 55,263.70 kwa mwaka 2019.

“Mwenendo huo unatokana na nchi hizi 2 kuendelea kuimarisha sekta ya usafilishaji kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa viwandani pamija na kuendelea kupunguza kikwazo visivyokuwa na kodi.”alisema Prof Kabudi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amewaomba wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika kumpokea Rais wa Malawi, Dkt Lazarus Chakwera

atakayekuja leo kwenye ziara yake ya siku tatu.

“Niwaombe watanzania tujitokeze kwa wingi kumpokeae na kumlaki mgeni wetu atakapo wasili na njiani atakapopita tunashukuru kwa heshima tuliopewa wakazi wa Dar es Salaam, tujitokeze kwa wingi kumpokea mgeni,” alisema Kunenge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles