-Lilongwe
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amewafuta kazi viongozi wa ngazi za juu akiwemo waziri wa Leba Ken Kandodo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kukabiliana na ugonjwa wa Covid 19 nchini humo.
Rais Chakwera alisema hatua hiyo ilifuatia ukaguzi kuhusu matumizi fedha ya kwacha za Malawi bilioni 6.2 ($ 7.8m; £ 5.6m) zidi ya kupambana na janga la Covid 19.
“Maafisa waliohusishwa na ubadhirifu katika ripoti ya ukaguzi, ofisini kwake na baraza la mawaziri, tayari wamekamatwa na kutakuwa na maafisa zaidi watakaokamatwa ndani ya utumishi wa umma.
“Siwezi kuwa na watu ndani ya baraza langu la mawaziri ambao wanatumia fedha zilizopangiwa kwa malengo tofauti” ,alisema Rais Chakwera.
Waziri wa Leba ameshtumiwa kwa kutumia vibaya kwacha 613,000 za Malawi zilizopangwa kutumiwa kupambana na Corona kwa kugharamia safari za kwenda Afrika Kusini.