29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa IFAD ampongeza JPM, atenga bilioni 120 kwa miradi ya kilimo

Elizabeth Joachim,Dar es Salaam

Rais wa Mfuko wa Kimataifa na Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Gilbert Houngbo amempongeza Rais Dk John Magufuli pamoja na serikali yake kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kukuza uchumi ikiwemo utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko huo.

Houngbo amesema hayo leo Mei 20 alipokuwa Ikulu Jijini Dar es Salaam kukutana rais Dk Magufuli na kufanya naye mazungumzo.

Amesema mfuko huo umetenga zaidi ya sh Billion 120 kwa ajili ya kuhifadhi miradi ya kilimo nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2020.

Aidha amesema baada ya kutenga fedha hizo mfuko huo unasubiri upande wa Tanzania kuainisha maeneo mahususi ya miradi ya kilimo ambako fedha zitaelekezwa, ameeleza kuwa ana matumaini miradi hiyo itafanikiwa kwa kuzingatia Tanzania ni nchi yenye amani na namna serikali ilivyo na dhamira ya maendeleo.

Naye Rais Magufuli, ameushukuru mfuko huo wa IFAD kwa ushirikiano na uhusiano ulioanza mwaka 1978 na kudumishwa kwa maslahi ya Watanzania.

Amesema fedha zilizotengwa katika mpango huo wa miaka mitatu zitaelekezwa katika maeneo yenye maslahi mapana ya sekta ya kilimo ikiwemo kuwezesha matumizi ya zana za kilimo katika uzalishaji, kuzalisha mbegu bora za mazao, kutatua changamoto za masoko ya mazao pamoja na kuboresha ufugaji.

Aidha Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuharakisha mchakato wa kusaminisha maeneo yatakayopokea fedha hizo ili uwekezaji wa mpango huo uanze.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles