23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

RAIS WA GUINEA BISSAU AMWAGA FEDHA KWA WACHEZAJI

BISSAU, GUINEA


Jose MarioRAIS wa nchini Guinea Bissau, Jose Mario, amemwaga fedha kwa wachezaji wa timu ya taifa ili kuwapa nguvu ya kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon, michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho.

Rais huyo aliitaka Serikali kutoa kiasi cha CFA milioni 12 kwa kila mchezaji ambazo ni sawa na 2,720,490 za Tanzania kwa kila mchezaji ikiwa ni furaha kuliona taifa hilo likishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

“Tumeamua kufanya hivi kuwapa furaha wachezaji wetu kwa sababu tumewapa kazi kubwa ya kutuwakilisha katika michuano hiyo mikubwa ya kimataifa nchini Gabon,” lilisema Shirikisho la Soka nchini Guinea Bissau.

Hata hivyo, shirikisho hilo limesema kwamba, limekubaliana na Serikali kuwapa ofa ya usafiri kwa baadhi ya wachezaji ili kuongeza nguvu ya kushangilia.

“Kazi yetu kubwa ni kutaka kuwafanya wachezaji wetu wajione kama wapo nyumbani katika michuano hiyo, tunaamini mashabiki wetu wakiwa wengi watatoa nguvu kwa wachezaji kufanya vizuri na tupo tayari kufanya hivyo.

Tunatarajia kukamilisha ndoto zetu, lengo kubwa ni kuhakikisha tunaweka historia katika soka kwenye michuano hii, ni mara yetu ya kwanza kushiriki na ndio maana tuna lengo kubwa la kuweka historia,” waliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles