30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS UHURU AZINDUA UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA KISUMU

KISUMU, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta akiwa katika ngome ya upinzani juzi alizindua ujenzi wa kituo cha mafuta chenye thamani ya Sh bilioni 1.7 za Kenya sawa na Sh bilioni 20 za Tanzania, ambacho anaamini kitasaidia taifa hilo kurudisha utawala wa soko la mafuta kikanda iliopoteza kwa Tanzania.

Ujenzi wa kituo hicho ulioanza Aprili mwaka huu umekamilika kwa asilimia 15 na kinatarajia kumalizika Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Rais kitaimarisha usambazaji wa mafuta kote katika kaunti ya Kisumu kwa lita bilioni moja kwa mwaka katika awamu ya kwanza hadi lita bilioni tatu kwa mwaka ifikapo mwaka 2028.

Aidha alisema kitakuza ufanisi wa usambazaji mafuta katika masoko ya Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo mwaka 2010 ulikuwa wa lita bilioni 2.4 na kupanda lita bilioni 3.5 mwaka 2016.

Pia itapunguza utegemezi wa matumizi ya malori katika barabara yenye shughuli nyingi ya Kisumu-Kampala  ambayo inalaumiwa kwa ajali nyingi za barabarani.

‘Mradi huu utatengeneza mamia ya ajira mpya kwa wakazi wa Kisumu na wakati huo huo kuchochea uchumi eneo kuzunguka Ziwa Victoria kwa kufungua njia za uchukuzi baina ya Kenya, Uganda na Tanzania,” Rais Uhuru alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hongera kwa mpangolio mzuri but intro and supporting para kwenye habari ya Rais wa marekani sio nzuri kuh uchaguzi wa keenya. Kiswahili kilichomika haisound vzr

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles