27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Uhuru awataka waguzi kusitisha mgomo

NAIROBI, Kenya

RAIS Uhuru Kenyatta ameamuru wauguzi kote nchini kusitisha mgomo wao na kurejea kazini mara moja, vinginevyo atawafukuza kazi.

Akizungumza jana mara baada ya kukutana na magavana wa majimbo Ikulu, kiongozi huyo wa nchi alisema wafanyakazi hao wa sekta ya afya wana muda hadi kesho kuwa wamerejea kazini.

Katika hotuba yake, Rais Uhuru alisema kwamba mgomo huo haupo kisheria na akawaagiza viongozi wa Serikali na Wizara ya Afya kumfukuza muuguzi yeyote ambaye atakuwa hajaripoti kazini hadi kesho.

 “Mimi kama Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya, ninawaagiza maofisa wote wa polisi kuchukua hatua ya kuwalinda wafanyakazi wa sekta ya umma ambao watataka kurejea kazini. Kwa wauguzi kama nilivyosema hapo mwanzo ambao hawataripoti kazini watafukuzwa moja kwa moja,” alionya Rais Uhuru.

Aliwalaumu wauguzi hao kwa kushindwa kuheshimu agizo la mahakama na akasema kwamba ni jukumu la kila raia wa Kenya kuheshimu sheria za nchi bila kujali nafasi zao katika jamii.

Huduma za afya nchini zilianza kuzorota tangu Februari 4, mwaka huu wauguzi walipoamua kuweka chini vitendea kazi vyao wakipinga kutotekelezwa mahitaji yao kama walivyokubaliana kabla ya kurejea kazini Novemba 2, mwaka juzi wakieleza kwamba hayajatekelezwa kikamilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles