27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Uhuru amchunguza jaji mwandamizi

NAIROBI, KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta ameunda mahakama maalumu kuchunguza mienendo ya Jaji wa Mahakama ya Juu zaidi, Jackton Ojwang.

Katika taarifa yake maalumu iliyotolewa juzi, Uhuru alisema kuwa kuondolewa kwa jaji huyo kutategemea matokeo ya uchunguzi huo wa mahakama.

Jopo la mahakama hiyo linaongozwa na mwenyekiti Jaji Alnashir Visram na wajumbe wakiwa majaji wastaafu, Festus Azangalala, Ambrose Weda, Andrew Bahati Mwamuye, Lucy Kambuni, Sylvia Wanjiku Muchiri na Amina Abdalla.

Uhuru alisema mienendo ya Jaji Ojwang inapaswa kuchunguzwa kutokana na maswali mengi yanayoulizwa juu yake.

Alisema hatua ya kuundwa kwa mahakama hiyo dhidi ya Ojwang, imetokana na ombi lililotolewa na Tume ya Huduma za Mahakama ya Kenya (CSJ).

Ombi hilo liliwasilishwa na kamati ya CSJ chini ya uenyekiti wa Nelson Oduor Onyango na wajumbe wengine wanane.

“Katika utekelezaji wa kazi zake, mahakama itaandaa na kuwasilisha ripoti na mapendekezo kwangu na baada ya hapo nitachukua uamuzi kulingana na mamlaka niliyopewa na sheria,” alisema Rais Uhuru.

 Katika ripoti iliyowasilishwa kwa Rais, Ojwang anashutumiwa kuwa na mienendo isiyofaa, kuibua migogoro isiyoendana na miiko ya kazi yake na ukiukaji wa kanuni za kazi yake.

Ojwang anaelezwa alikuwa mmoja wa majaji wa Mahakama ya Juu zaidi walioendesha kesi katika Kaunti ya Migori ilhali ikifahamika ni mshirika wa karibu wa Gavana wa kaunti hiyo, Okoth Obado.

Wajumbe tisa wa CSJ walisema Obado aliweka lami kwenye barabara inayoelekea makazi binafsi ya kijijini ya Jaji Ojwang, kitu kinachotia shaka.

Kwa maoni yao, Ojwang angepaswa kuifahamisha mahakama na wadau wote juu ya ushirika wake wa karibu, kwa maana ya masilahi aliyonayo kwa gavana huyo, lakini hakufanya hivyo hadi alipopingwa.

 â€œKutokana na tuhuma zilizomkabili Jaji Ojwang, tume ya JSC ilichunguza kwa makini kwa marefu na mapana na kubaini kuwa kuna sababu za kutosha za kumwomba Rais kuunda mahakama ya kumwondoa madarakani, na kuidhinisha ombi kulingana na sheria,” alisema Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu, David Maraga.

 Aidha Rais Uhuru amewateua wanasheria Paul Nyamodi na Stella Munyi kuwa washauri wa  kusaidia mahakama hiyo maalumu kwa uchunguzi wa Ojwang.

 Alisema Peter Kariuki na Josiah Musili watahudumu pamoja kama makatibu wa mahakama hiyo maalumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles