33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Rais Trump azindua rasmi kapmeni za urais

Washington, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump amefanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni tangu nchi hiyo ilipoweka amri ya kutotoka nje kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, huku akiwa mbele ya watu wachache badala ya umati mkubwa wa watu uliotarajiwa.

Trump alikua amejigamba mapema wiki iliyopita kwamba karibu watu milioni walikua wameomba tiketi za kuhudhuuria mkutano huo katika eneo la benki ya Tulsa katika kituo cha Oklahoma.

Lakini viti 19,000 vya uwanja huo viliachwa wazi bila watu na mipango yake ya kuhutubia watu ambao alitarajia wangelazimika kukaa nje iwapo uwanja ungefurika ilibidi iachwe.

Kumekua na hofu juu ya kuendesha mikutano ya kisiasa wakati wa janga la corona.

Virusi vya corona lilikua ni suala moja lililozungumziwa na Trump katika mkutano huo, katika hotuba yake iliyodumu karibu saa mbili kwa wafuasi wake waliokua wakimshangilia, katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha Republican.

Trump alisema kuwa aliwaambia maofisa kupunguza upimaji wa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 kwa sababu watu wengi sana walikua wanapatikana na virusi, lakini baadae katika hotuba hiyo akasema maneno hayo ni mzaha tu.

Wale waliohudhuria mkutano wa kampeni walilazimika kusaini makubaliano ya kuilinda timu ya kampeni ya Trump kwamba haitawajibika na ugonjwa wowote iwapo watapata maambukizi.

Saa kadhaa kabla ya tukio hilo kuanza, maofisa walisema kuwa wahudumu sita wa kampeni ya Trump walipatikana na maambukizi ya virusi vya corona.

Hata hivyo, haijawa wazi ni kwanini ni watu wachache waliojitokeza kuliko ilivyotarajiwa. Bwana Trump aliwaelezea wale waliokuwa uwanjani kumsikiliza kama “wapiganaji”, huku akiwalaumu waandamanaji na vyombo vya habari kwa kuwafukuza wafuasi wake.

Kulikua na kizaazaa nje ya uwanja wa mkutano, lakini hapakua na matatizo makubwa yaliyojitokeza.

Trump aliutumia mkutano huo kuwashambulia wapinzani wake wa Democratic wakati akikabiliana nakelel kuhusu janga kubwa la kiafya na mgogoro wa kiuchumi pamoja na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi ambayo yamelifagia taifa ghilo katika wiki za karibuni.

Mrepublican huyo alidai ushindi dhidi ya janga hilo ambalo limewauwa karibu Wamarekani 120,000.

Trump alimshambulia mpinzani wake katika uchaguzi wa 2020, Mdemocrat Joe Biden, akimtaja kuwa “kibaraka wa watu wa siasa kali za mrengo wa kushoto.”

Rais huyo alipuuza kitisho kuwa mkutano huo wa jioni, huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliohudhuria huenda ukachochea mlipuko mpya wa virusi vya corona, na kupuuza onyo lililotolewa la maafisa wa afya wa Tulsa na manispaa ya mji huo.

Aliwaambia wafuasi wake kuwa Marekani imewapima watu milioni 25, ikiwa ni idai kubwa zaidi kuliko nyingi nyingine yoyote.

“Ukifanya vipimo kwa kiwango hicho, utakuta watu wengi zaidi, utakuta visa vingi zaidi,” alisema Trump.

Kabla ya kupanda jukwaani, waandamanaji wa vuguvugu la Black Lives Matter, wanaopinga ukatili wa polisi na ubaguzi dhidi ya Wamarekani Weusi, waliandamana kwa amani kumpinga kiongozi huyo wanayembebesha lawama za kuchochea chuki dhidi ya walio wachache katika miaka minne ya utawala wa wake.

Wafuasi wa Trump walikusanyika kwenye uwanja wenye viti 19,000 na mwandishi wa habari wa Shirika la AP aliripoti kwamba wengi wao hawakuwa wamevaa barakoa licha ya onyo la maofisa wa afya.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles