24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

RAIS TRUMP AWAKASIRISHA WAINGEREZA

LONDON, UINGEREZA


HATUA ya Rais wa Marekani, Donald Trump, aliyeko ziarani nchini Uingereza kumkosoa Waziri Mkuu, Theresa May kuhusu mpango wa Brexit, imeibua hasira miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo.

Ukosoaji wa Trump umewakasirisha Waingereza, ambapo Naibu Waziri Mdogo, Sam Gyimah, amemtaka Rais Trump kujifunza adabu.

Gyimah, ambaye ni Naibu Waziri Mdogo wa Masuala ya Utafiti katika Vyuo Vikuu na Sayansi Uingereza, ameandika katika mtandao wa Twitter akihoji nidhamu ya Rais Trump dhidi ya wananchi wa Uingereza.

Katika mkesha wa mkutano kati yake na May, Trump alisema kuwa, hatua ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya huenda itavunja matumaini ya mahusiano ya kibiashara kati ya mataifa hayo.

Akitetea uamuzi huo, Waziri Mkuu May amesema hawezi kuburuzwa na Umoja wa Ulaya kinyume na matakwa ya wananchi wake walioamua kujiondoa kwenye Umoja huo.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha wa Uingereza, Phillip Hammond, amesema: “Trump hajawa na nafasi ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, lakini ana matarajio makubwa ya kupata fursa hiyo. Mazungumzo hayo yatalenga kutazama jinsi ya kupanua biashara na uwekezaji kati ya Uingereza na Marekani.”

Hammond aliwaambia hayo waandishi wa habari kabla ya mkutano na mawaziri wa fedha wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya jijini Brussels.

Ziara ya Trump imefanyika katika kipindi ambacho Waziri Mkuu May anapitia wakati mgumu, baada ya mawaziri wake, David Davis (Waziri wa Ulinzi) na Waziri wa Masuala ya Nje, Boris Johnson, kujiuzulu, wakipinga kusuasua kwa mpango wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Matamshi kama hayo kwa Rais wa Marekani yamechochea kushusha thamani ya sarafu ya sterling. Alipoulizwa kuhusu matamshi hayo, msemaji wa Waziri May alisema kuwa, atafanya kikao na rais huyo wa Marekani na kujadili msimamo wake huo.

KWA HABARI ZAIDI PATA NAKALA YAKO LA GAZETI LA MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles