23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia ziarani nchini China

Na Mwandishi wetu

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi Nchini China kuanzia leo September 02 hadi September 06, 2024 kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC) utakaofanyika Jijini Beijing.

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga imesema katika ziara hiyo Rais Dk. Samia atakutana na mwenyeji wake Rais wa China, Xi Jinping, kwa mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na China ulioasisiwa miaka 60 iliyopita.

Marais hao wawili pamoja na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema watashiriki na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano ya Uboreshaji wa Reli ya TAZARA.

Pamoja na mambo mengine, miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kupewa kipaumbele kwenye Mkutano wa FOCAC ni uendelezaji wa miundombinu, kukuza uwekezaji, uendelezaji wa viwanda, kilimo cha kisasa na amani na usalama, Rais Dk. Samia anatarajia kuwa miongoni mwa wakuu wa nchi watakaohutubia ufunguzi wa Mkutano wa FOCAC akizungumza kwa niaba ya Kanda ya Afrika Mashariki.

Pamoja na mkutano huo, katika kukuza biashara na uwekezaji, Rais Dk. Samia atakutana na makampuni na Wawekezaji kutoka China kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles