24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia ni kielelezo cha Afrika Mpya

Na Mariam Mniga

Watu wa nchi mbalimbali za barani Afrika wamedai uapisho wa Samia Sululu
Hassan kuwa na rais wa kwanza Mwanamke kwa Tanzania ni ishara kuwa bara la Afrika lina achana na mila na desturi za kizamani za kuzarau na kumuhusisha Mwanamake na shughuli za ndani na za kulea watoto na kwamba bara hilo linaonyesha linatambua umuhimu wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake.

Katika mahojiano ya simu na waafrika kutoka nchi za Sudani, Uganda, Zambia, Kenya, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Nigeria, Kenya, Cameroon, Gabon, zimbabwe, Africa ya Kusini na Rwanda wamedai kitendo cha Rais Samia Suluhu ni kuithibitishia dunia kuwa Afrika iko tayari na inaamini Mwanamke kuwa na uwezo wa uongozi katika ngazi za juu ndiyo maana katika nchi mbalimbali za bara hilo zimekuwa imani na zikiwateua wanawake kushika nyadhfa mbalimbali za kitaifa na kimataifa kama vile umakamu wa raisi, uwaziri, ubunge na wameweza kuwakilishwa na wanawake wa mataifa hayo katika jumuiya na taasisi za kimataifa.

Victor Joshua kutoka Nigeria ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Utah, ambacho ni chuo Kikuu cha Kimarekani chenye tawi lake nchini Korea ya Kusini amesema ongezeko la idadi ya wanawake katika nyanja za juu ni dalili ya kuwepo kwa Demokrasia katika nchi hizo.

Rais Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Na ameongea kwa kusema “Hii ni matokeo ya mkutano wa wanawake uliofanyika mjini Beijing mwaka 1995…wanawake wanajulikana kuwa wasuluhishi wazuri kwa hiyo Afrika ina imani na Rais Samia Sululu”

Wafrika wamedai kuwa na imani na Rais mpya wa Tanzania kwa kuwa wanawake kwa ujumla wanajulikana kuwa ni wasuluhishi wazuri.

Katika mahojiano hayo wamedai maraisi wanawake wanauwezo na ni watendaji wazuri na pia wameweka historia ya kuchukua madaraka ya nchi zao wakati zilipokuwa zinapitia wakati mgumu cha kisiasa na kiuchumi na wameweza kuimalisha ulinzi na usalama na kuweka muelekeo mpya unaodhamini haki za binaadamu.

Samia amechukua madaraka wakati Tanzania inapitia changa moto za ugonjwa wa homa ya mapafu, yaani covid- 19 na machafuko ya kisiasa na matishio ya kijasusi katika nchi za jirani kama vile msumbiji, Congo DRC na kenya, Somalia Sudani na Ethiopia.

Nchi nyingine za Afrika ambazo zimekuwa na maraisi Wanawake ni Malawi, Jamuhuli ya Afrika ya kati, Ethiopia, Liberia, Burundi, Malawi na Mauritius. Maraisi hao kabla ya kushika nafasi hizo walikuwa Mawaziri na Makamo wa Maraisi katika nchi zao, kwa kuwa nchi hizo zinatambua uwezo wa wanawake katika uongozi.

Irene Dawa, Mwanafunzi wa Udakari wa Philosophia-Phd katika chuo kikuu cha Durban huko South Africa amesema “Nchi za aAfrika ziko tayari kuongozwa na wanawake, kama wangekuwa hawaamini uwezo wa mwanamke katika uongozi wasengekuwa wanateuliwa kushika nafasi za juu ikiwamo nafasi ya umakamo wa rais,” anasema.

Raisi wa kwanza kushika nafasi uraisi baada ya kushinda uchaguzi katika bara la Afrika ni aliyekuwa rais wa Liberia, Mama Hellen Sirleaf Johnson ambaye pia alikuwa Waziri wa fedha katika utawala wa Samwel Doe.

Joyce Banda

Joyce Banda alichukua nafasi ya urais wa Malawi kufuatia kifo cha rais wa chini hiyo bingu mutharika Mwaka 2012.

Raisi wengine wa kike ni catherine samba- panza ambaye alikuwa meya wa bangui ambao ni mji mkuu wa jamuhuri ya afrika ya kati( CAR) alichukua nafasi hiyo kama rais wa mpito kufuatia kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo, Michel Djotodia 2014.
Rais wa sasa wa Ethiopia Mama Sahle- Work Zewde alikuwa Balozi wa Ethiopia nchini Senegal na baadaye Djibuti, Ufaransa, Tunisia na Morocco. Kabla ya kuchukua nyazifa huo mama Zewde aliteuliwa na rais wa nchi hiyo kuwa mwakilishi katika ofice ya umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za Africa.

Mama Slyvie Kining alikuwa Waziri Mkuu wa Burundi na baadaye akawa rais baada ya wa nchi hiyo, Melchior Ndadaye kuuwawa kwa kupigwa risasi wakiwemo na maafisa wengine wa serikali yake.

Ellen Sirleaf Johnson

Rais wa Mauritius mama Ameenah Gurib-Fakim ni raisi mwengini wa afrika aliyechaguliwa kwa kura nyingi zilizopigwa na bunge la nchi hiyo mwaka 2015, alitwaa madaraka hayo hufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa raisi wa nchi hiyo bw. Kailash Purryag.

Mama Samia sululu aliapiswa kuwa raisi wa awamu ya sita kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa tanzania kupitia Chama Cah Mapinduzi(CCM) Hayati, Dk. John Pombe Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles