27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kufungua mkutano wa Dira ya Taifa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua  Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Maendeleo ya Taifa utakaofanyika Disemba 9, 2023 katika Kituo chaMikutano cha  Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Disemba 1, 2023 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,  Profesa Kitila Mkumbo amesema  jumla ya wadau 971 wamealikwa kushiriki mkutano huo na utahudhuriwa na makundi maalum na viongozi mbalimbali nchini.

Amesema lengo kuu la mkutano  huo ni kuzindua, kupokea  na kujadili  taarifa  ya  kitafiti ya tathmini  ya utekelezaji wa dira ya maendeleo  ya Taifa  2025.

“Dk. Samia atazindua rasmi timu kuu ya kitaalam ya dira na kamati ya usimamizi wa dira pamoja na nyenzo za kidigitali zitakazotumika katika kukusanya  maoni ya wadau, “amesema Profesa Mkumbo.

Amesema taarifa ya kitafiti ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 pamoja na mengine na imeainisha mafanikio  yanayopatikana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa dira hiyo.

Amesema dira hiyo ilianza kutelezwa mwaka 2000 na inafikia mwisho wake mwaka 2025, pamoja  na mafanikio  mengine  taarifa  ya tathimini  inaonesha pato la mtanzania limeongezeka kutoka dola za Kimarekani 399.5 mwaka 2000 hadi kufikia dola 1200.

“Tanzania imefikia asilimia 124 ya kujitosheleza kwa chakula ilikulinganishwa na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo mwaka 2025 na kupunguza  vifo vinavyotokana na uzazi kutoka vifo 760 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2000 hadi kufikia 104 mwaka  2022 ikiwa tumevuka lengo la kufikia  vifo 265 ifikapo  mwaka 2025 ni matokeo kamili ya tathimini hii,”amesema.

Ameongeza kuwa wameanza mchakato wa kuandaa  Dira mapya ya  2050, huku akiwaomba wananchi kufuatilia mchakato huo na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao kuhusu Tanzania  waitakayo katika miaka ijayo.

Aidha amesema kwa kuwa mkutano huo unafanyika  siku ya uhuru Rais Samia atatumia siku hiyo kutoa ujumbe maalumu  katika maadhimisho miaka 62 ya uhuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles